Home Kimataifa CHELSEA VS PSG: MECHI PREVIEW NA VIKOSI VIANAVYOTARAJIWA KUANZA

CHELSEA VS PSG: MECHI PREVIEW NA VIKOSI VIANAVYOTARAJIWA KUANZA

708
0
SHARE

Chelsea vs PSG 4

Macho yote leo yataelekezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge wakati wa mchezo wa marudiano wa Champions League kati ya Chelsea dhidi ya PSG. Mechi ya kwanza ilimalizika kwa PSG kushinda kwa mabao 2-1ikiwa nyumbani Ufaransa.

Ni mchezo mgumu sana kwa timu zote mbili, hii ni mara ya tatu ndani ya misimu mitatu Chelsea na PSG kukutana kwenye mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Stamford Bridge kuamua nani atasonga mbele kwa hatua inayofuata.

Msimu uliopita PSG ilishinda kwenye muda wa nyongeza licha ya of Zlatan Ibrahimovic kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Msimu wa 2013-14, Demba Ba alikuwa shujaa wa Chelsea baada ya kufunga bao la kuipeleka Chelsea kwenye hatua ya robo fainali chini ya Mourinho.

Licha ya PSG kuwa katika kiwango bora kwenye ligi ya Ufaransa, haikuwa rahisi kwao kupata ushindi mbele ya Chelsea kwenye mchezo wa kwanza.

Free-kick ya Zlatan Ibrahimovic iliyomgonga Jon Obi Mike na kuzama wavuni lakini Mikel alisawazisha bao hilo kabla ya timu hizo kwenda mapumziko. Edinson Cavani akitokea benchi akaipa ushindi klabu yake ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Kuelekea mchezo huo, klabu hiyo ya Ufaransa inawashambuliaji hatari kwenye klabu yao lakini wanakutana na Chelsea yenye safu ngumu ya ulinzi chini ya Guus Hiddink licha ya kukabiliwa na majeruhi kwa baadhi ya nyota wa nafasi hiyo.

The Blues watakosa huduma ya nahodha wao John Terry wakati Diego Costa yeye anatarajiwa kurudi uwanjani baada ya kukosa mchezo dhidi ya Stoke akiwa anakabiliwa na majeruhi.

Chelsea inatarajiwa kuanza na kikosi kilele ambacho kilianza kwenye mchezo wa kwanza jijini Paris huku makinda Bertrand Traore, Kenedy na Ruben Loftus-Cheek wakiwa machaguo ya ziada kwenye benchi.

Chelsea itatemea sana huduma ya Eden Hazard ambaye kwasasa anaonekana kufanya vizuri. Mbelgiji huyo ameanza kuonesha dalili za kuimarika siku za hivi karibuni.

PSG wametaja kikosi kikali ambacho Serge Aurier ni mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo huo.

Tarajia kumuona Zlatan Ibrahimovic kuongoza safu ya ushambuliaji wakati Cavani yeye atatokea benchi. Uwepo wa Lucas Moura na Angel Di Maria utamfanya Marco Verratti kuanzia benchi.

Kikosi cha Chelsea kinachotarajiwa kuanza: Thibaut Courtois, Cesar Azpilicueta, Gary Cahill, Branislav Ivanovic, Baba Rahman, Jon Obi Mikel, Cesc Fabregas, Willian, Eden Hazard, Oscar na Diego Costa.

Kikosi cha PSG kinachotarajia kuanza: Kevin Trapp, Marquinhos, David Luiz, Thiago Silva, Maxwell, Blaise Matuidi, Thiago Motta, Marco Verratti, Lucas Moura, Angel Di Maria na Zlatan Ibrahimovic.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here