Home Kimataifa Cristiano Ronaldo Kuwa Baba Kwa Mara Ya Pili?

Cristiano Ronaldo Kuwa Baba Kwa Mara Ya Pili?

1056
0
SHARE

Gazeti la kireno la Correio da Manha wameanzisha tetesi kubwa, wakidai kwamba Cristiano Ronaldo anatarajia kuwa baba kwa mara ya pili.

 Mpaka sasa taarifa hii inaonekana kuwa tetesi, lakini imekuwa ikizidi kukua kwenye mitandao ya kijamii jambo liloanza baada ya Cristiano Ronaldo kushangalia moja ya magoli yake manne vs Celta Vigo kwa kuweka mpira ndani ya jezi yake kwenye eneo la tumbo.

Ushangiliaji wa aina hii umekuwa maarufu kwa kutumiwa na wanasoka wengi baada ya kufunga magoli – wakitoa ishara kwamba wanatarajia kuwa na wenza wao ni wajawazito.

 Correio da Manha wameripoti kwamba wamejaribu kupata ufafanuzi juu ya issue hiyo kwa Ronaldo, mama yake, na dada zake lakini wote waligoma kuzungumzia suala hilo.

Mpaka sasa hakuna mwanamke ambaye amehusishwa na tetesi hizi, na Correio da Manha wanaeleza Ronaldo anaweza kumficha mama wa mtoto wake kama ilivyo kwa mwanae wa sasa Cristiano Jr

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here