Home Kitaifa YANGA YARUDI KILELENI KWA FUJO, YAITOA SIMBA BAADA YA SAA 48

YANGA YARUDI KILELENI KWA FUJO, YAITOA SIMBA BAADA YA SAA 48

821
0
SHARE

????????????????????????????????????

Ushindi wa bao 5-0 walioupata Yanga dhidi ya African Sports ya barabara ya 12 Tanga, uwewarejesha kwenye nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Simba waliodumu kwenye nafasi hiyo kwa saa 48 baada ya ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Mbeya City, wanashushwa hadi nafasi ya pili baada ya kuzidiwa pointi 2 na wapinzani wao wa jadi. Yanga ilikuwa na pointi 47 kabla ya ushindi wa leo sasa wamefikisha pointi 50 wakiiacha Simba na pointi zake 48.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Kelvin Yondani, Donald Ngoma, Amis Tambwe ambaye amefunga magoli mawili pamoja na Anthony Matheo.

Takwimu muhimu kuzifahamu

  • Klabu ya Yanga imefikisha pointi 50 pointi mbili zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 48 huku timu hizo zikiwa na idadi sawa ya michezo (21) wakiizidi Azam FC kwa mchezo mmoja ambayo ipo nafasi ya tatu kwa pointi 47.
  • Pato Ngonyani ameanza kwa mara ya pili kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga msimu huu wakati inacheza na African Sports, Ngonyani alianza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza wakati Yanga ilipocheza na Simba.
  • Matheo Anthony amefunga bao lake la kwanza kwenye ligi ya Vodacom Tanzania tangu alipojiunga na Yanga, nyota huyo wa zamani wa KMKM ya visiwani Zanzibar alifunga bao la kwanza akiwa Yanga kwenye mchezo wa FA dhidi ya Friends Rangers lakini leo amefunga kwenye ligi.
  • Amis Tambwe amefunga bao mbili na kufikisha magoli 17 na kumpita mshambuliaji wa Simba mganda Haisi Kiiza kwa bao moja ambaye hakufunga bao katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Yanga pamoja na ule wa Mbeya City hivyo kubaki na magoli yake 16 nyuma ya Tambwe.
  • Mara ya mwisho Yanga kushinda kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa ligi ilikuwa ni February 7, 2016 walipoitandika JKT Ruvu kwa bao 4-0 kabla ya leo kuifunga African Sports kwa idadi kama hiyo ya magoli.
  • African Sports na Mgambo JKT ni timu za tanga ambazo zote zimefungwa bao 5 kwenye uwanja wa taifa. Simba waliifunga Mgambo kwa bao 5-1 February 2, 2016, Simba na Yanga zinautumia uwanja wa taifa kama uwanja wao wa nyumbani wakati African Sports na Mgambo JKT wao wakiutumia uwanja wa Mkwakwani kama uwanja wao wa nyumbani.
  • African Sports inaendelea kusalia kwenye nafasi ya 15 ikiwa na pointi 17 huku ndugu zao wa jiji moja la Tanga Coastal Union wakiburuza mkia kwa kukuwa nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here