Home Kimataifa Real Madrid vs AS Roma: Madrid kuvunja mwiko dhidi ya Waitaliano na...

Real Madrid vs AS Roma: Madrid kuvunja mwiko dhidi ya Waitaliano na Kufuzu Robo fainali kwa mara 6 mfululizo?

682
0
SHARE

Real Madrid CF inakutana na AS Roma leo katika mchezo wa pili wa raundi ya 16 bora wakiwa wameshaingiza mguu mmoja ndani kwenye robo fainali kwa msimu wa sita mfululizo.image

• Madrid wamepoteza mechi zao mbili za raundi ya pili katika hatua tofauti za UCL dhidi ya timu za Serie A, lakini magoli ya Cristiano Ronaldo na Jese yamewaweka sehemu nzuri katika kuvuka kwenda robo fainali.

• Kwa Zinédine Zidane, hii ndio mechi ya kwanza ya UEFA Champions League katika uwanja wa nyumbani akiwa mwalimu wa timu ambayo huko nyuma mwaka 2002 alishinda nayo taji la michuano hii, akifunga goli katika fainali. Alimrithi Rafa Benitez mnamo January 2016.

• Roma pia wamefanya mabadiliko ya kocha mwanzoni mwa mwaka huu baada ya Rudi Garcia kuondolewa na nafasi yake kujazwa na Luciano Spalletti, ambaye aliwahi kuiongoza timu kuiondoa Madrid kwenye michuano hii mara ya mwisho walipokutana.

1455739950058_lc_galleryImage_epa05166980_Real_Madrid_sMechi Zao Zilizopita
• Kabla ya msimu huu vilabu hivi viliwahi kukutana mara 8 katika michuano ya ulaya, Madrid wakishinda mara 4, Roma wakishinda 3 na mara moja sare.

• Mara ya mwisho wawili hawa kukutana kwenye mechi ya mashindano ilikuwa katika UEFA Champions League raundi ya 16 bora msimu wa 16 in 2007/08 wakati wa kikosi cha Spalletti kiliposhinda 2-1 nyumbani na ugenini.

 

TAARIFA ZA VIKOSI

510884994
• Casemiro na Ramos wanaweza wakapata adhabu ya kutocheza mechi inayofuatia ya michuano hii endapo leo watapata kadi za njano, kwa upande wa Roma De Rossi na Radja Nainggolan nao wapo kwenye hatari kama hiyo.

• Benzema alipata majeruhi ya misuli kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Atletico na anategemewa kuikosa mechi ya leo, Luka Modric pia ana majeruhi ya enka, wakati Marcelo na Bale ambao hawakucheza mechi ya kwanza walirejea dimbani wikiendi iliyopita dhidi ya Celta Vigo.

• De Rossi alipata majeruhi na hatokuwepo uwanjani kwa wiki 4, Kevin Strootman, yupo fiti baada ya kupona majeruhi yake ya muda mrefu ya goti, na alicheza mechi ya kwanza mwishoni mwa mwezi uliopita – hata hivyo kiungo huyo hayupo katika cha Champions League cha AS Roma.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here