Home Ligi EPL HIDDINK AVUNJA REKODI ILIYODUMU KWA MIAKA 21 EPL

HIDDINK AVUNJA REKODI ILIYODUMU KWA MIAKA 21 EPL

621
0
SHARE

FBL-EUR-C1-CHELSEA-PRESSER

Guus Hiddink ameweka rekodi mpyandani ya Premier League kufuatia sare iliyopata timu yake ya kufungana bao 1-1 na Stoke City siku ya Jumamosi.

Bertrand Traore alianza kuifungia Chelsea bao la kuongoza kipindi cha kwanza lakini goli la dakika za lala salama lililofungwa na Mame Biram Diouf liliweza kuwapa the Potters pointi moja wakiwa ugenini.

Kocha wa the Blues Hiddink anasababu moja ya kutabasamu baada ya mholanzi huyo kuweka rekodi ya kuwa kocha ambaye ameiongoza timu katika michezo mingi bila kupoteza mchezo kwenye ligi ya EPL. Akiwa ameiongoza Chelsea mechi 12 bila kupoteza, anavunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na kocha wa zamani wa Nottingham Forest Frank Clark ambaye timu yake haikupoteza michezo 11 chini yake kwenye msimu wa 1993-94.

Sare hiyo imeiacha Chelsea ikisalia kwenye nafasi yake ileile ya 10 kwenye ligi ikiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Man City ambayo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo. Kama Chelsea ingeshinda mchezo huo ingepanda hadi nafasi ya saba na kuiondoa Stoke City.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here