Home Kitaifa BAADA YA TWIGA STARS KUCHAPWA NYUMBANI, KOCHA ATOA SABABU

BAADA YA TWIGA STARS KUCHAPWA NYUMBANI, KOCHA ATOA SABABU

538
0
SHARE
Nasra Juma -kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars)
Nasra Juma -kocha wa  timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars)
Nasra Juma -kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars)

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimekubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Baada ya mchezo huo kumalizika, kocha wa Twiga Stars Nasra Juma amesema kukosa ligi ya wanawake Tanzania ni moja ya sababu inayopelekea timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano.

“Mchezo ulikuwa mzuri na wachezaji wangu wamejituma kwa kiwango kikubwa hali haikuwa mbaya sana, timu pinzani imeweza kutumia mapungufu na imeweza kufunga magoli ambayo yote yamechangiwa na sisi wenyewe na kama tunavyosema makosa yanayotokea ndiyo yanasababisha magoli”, amesema Nasra Juma ambaye amechukua nafasi ya Rogasian Kaijage aliyejiuzulu.

“Nilipata pigo moja kubwa sana captain wangu Sophia Mwasikili aliumia wakati tunafanya warm-up aliumia uti wa mgongo na alikuwemo kwenye kikosi kinachoanza tukalazimika kufanya mabadiliko ya harakahakara”.

“Baada ya kuona mmchezo huu, tunarudi tena kambini kufanya mazoezi ya wiki mbili na tutaendelea kuongoza mazoezi ya nguvu zaidi ili wachezaji waweze kuhimili vishindo vya mechi ya ugenini”.

“Kwa bahati mbaya sana hapa nchini hatuna ligi ya wanawake na timu hii haijacheza tangu irudi kwenye michuano ya All African Games mwezi September mwaka uliopita kwahiyo hiyo inachangia kwa kiasi flan wachezaji wetu kukosa mbinu za kukabiliana katika michezo kama hii”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here