Home Ligi EPL WACHEZAJI WALIOBEBA NDOO YA EPL BAADA YA KUONDOKA ARSENAL

WACHEZAJI WALIOBEBA NDOO YA EPL BAADA YA KUONDOKA ARSENAL

741
0
SHARE

Fab-Parsie

Ni miaka 12 sasa Arsenal wanaweza kuadhimisha toka washinde kombe la Ligi kuu nchini Uingereza kwa mara ya mwisho, ni kitu kinachowauma sana sio mashabiki tu wa klabu hiyo lakini hata wachezaji pia.

Ndiyo, mtu anaweza kusema kuwa Vijana wa Arsene Wenger ni wapinzani sahihi wa kombe wa kombe la Ligi kuu Uingereza msimu huu kutokana ana wapinzani wake wa muda mrefu Chelsea na Manchester United wote wakiwa nje ya Top Four.

The Gunners kwa sasa wameachwa pointi sita wakiwa katika nafasi ya tatu na vinara wa ligi hiyo Leicester City, labda tusubiri na tuone kama vijana hao wa kasikazini mwa Jiji la London wataweka tabasamu katika nyuso zao kwa kuchukua kombe la Ligi kuu Uingereza ifikapo mwezi wa tano mwaka huu.

Kuna baadhi ya wachezaji waliojaribu kusubiri kama Arsene Wenger,wakaamua kutimka Arsenal na kujiunga na vilabu vingine vya Ligi kuu Uingereza na wakafanikiwa kuchukua Kombe la Ligi kuu Uingereza japo kuwa sio wote waliofanikiwa,wafuatao ni wachezaji watatu waliotimka Arsenal na kufanikiwa kuchukua ndoo ya EPL.

Samir Nasri- Manchester City

Nasri 7

Kiungo huyu Mfaransa alijiunga na Arsenal akitokea Marseille mwaka 2008 akisaini mkataba wa miaka minne , lakini hakukaa kwa muda mrefu pale Emirates ambapo yeye na mwenzie Gael Clichy walipoamua kuondoka na kujiunga na Manchester City mwaka 2011, ambapo walifanikiwa kujipatia medali ya Ligi kuu ya Uingereza katika msimu wao wa kwanza tu baada ya kuhama Arsenal.

Robin Van Persie- Manchester United

Nani 3

Baada ya kumaliza msimu wa 2011-2012 akiwa mfungaji bora wa Ligi kuu ya Uingereza akiwa amewafungia Arsenal goli 30,Van Persie alitangaza kuwa hawezi kusaini mkataba mpya na Arsenal na hivyo kuhitimisha huduma yake ya miaka saba dhidi ya The Gunners akiwa hana kombe lolote.

Siku chache baadae Mholanzi huyo akafanikiwa kujiunga na Mashetani wekundu Manchester United ambapo alifanikiwa kufuata nyao za wachezaji wenzake wa zamani kina Nasri na Gael Clichy kwa kunyakua kombe la Ligi kuu Uingereza katika msimu wa kwanza baada ya kuondoka Arsenal.

Cesc Fabregas- Chelsea

Fab

Kama kuna mchezaji yeyote mashabiki wa arsenal hawatakuja kumsahau ni Cesc Fabregas, Mhispaniola huyu alijiunga na Arsenal mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 16 akitokea Academy ya Barcelona La Masia.

Aliendelea kukua na kuwa moja ya viungo boora Duniani na alichaguliwa kuwa nahodha wa Klabu hiyo mwaka 2008 alikuwa akiibusu nembo ya Arsenal kila alipokuwa akifunga goli na kwa mara akadhaa alikaririwa akimuita Kocha wa Arsenal Arsene Wenger baba yake wa pili.

Lakini ukame wa makombe ulimfanya asiweze kuendelea kukaa katika klabu ambayo alikuwa akichukuliwa kama shujaa.

Barcelona walituma ofa mara nyingi katika kipindi chake akiwa Arsenal lakini walifanikiwa kumnasa mwaka 2011 katika moja ya uhamisho unoweza kuhesabika kama uhamisho wenye usumbufu na utata mkubwa katika historia ya soka Duniani.

Muda wake Barcelona haukuenda kama ulivyotakiwa, Fabregas aliamua kurudi Uinghereza na Kocha wa zamani wa Chelsea Mreno Jose Mourinho alifanikiwa kumnasa kabla ya Kombe la Dunia mwaka 2014.

Na kile ambacho Mfaransa alishindwa kumpa Fabregas ndani ya miaka nane Mourinho alimpa Cesc fabregas ndani ya mwaka mmoja baada ya Chelsea kushinda kombe la Ligi kuu Uingereza katika msimu wa kwanza alipojiunga Fabregas.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here