Home Ligi EPL Je Van Gaal ataumaliza msimu vizuri? Aiongoza United kushinda mechi ya 4...

Je Van Gaal ataumaliza msimu vizuri? Aiongoza United kushinda mechi ya 4 mfululizo 

652
0
SHARE

img_3997.jpg

Mapema wiki iliyopita hakuna shabiki wa ambaye alikuwa anaamini timu yake ingeweza kupata matokeo chanya katika mechi 4 zilikuwa zinafuatana mfululizo za michuano tofauti, kutokana kiwango cha timu yao na udhaifu wa kikosi hicho kilichojaa majeruhi.

Lakini chini ya kocha ambaye anaripotiwa kwamba siku zake za kuendelea kuwa mkufunzi mkuu wa timu hiyo zinahesabika – Manchester United imefanikiwa kushinda mechi zote zilizokuwa mbele yao.

Baada ya kufungwa 2-1 na FC Mityjlland wiki mbili zilizopita, United waliifungua wiki iliyopita na ushindi wa 3-0 dhidi ya Shrewbury FC katika mchezo wa raundi ya 5 ya kombe la FA.
Alhamisi ya wiki iliyopita Van Gaal na vijana wake wakawa na mtihani wa kugeuza matokeo ya 2-1 dhidi ya FC Mityjlland baada ya kufungwa nchini Denmark – na kwa bahati mbaya majeruhi yakazidi kuongezeka, mshambuliaji tegemeo Antonio Martial akaumia wakati akipasha misuli kabla ya mchezo. Nafasi yake akapewa kinda kikosi cha pili Marchs Rashford ambaye aling’ara usiku huo kwa kufunga magoli katika ushindi 5-0 dhidi ya klabu hiyo ya kidenishi.
 Mtihani uliofuatia ulikuwa jumapili iliyopita dhidi ya Arsenal ambao waliingia kwenye mchezo huo wakipewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya kuitandika United iliyo kamili 3-0 katika mchezo wa kwanza, alikuwa yule yule kijana wa Marcus Rashford akapiga tena mbili na Hererra akafunga lingine na kuwapa United ushindi wa 3-2 na kuamsha ndoto za Van Gaal kumaliza ndani ya Top 4.

Mechi ya 4 ilikuwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Watford katika mfululizo wa ligi kuu ya England.
 Goli pekee la Juan Mata katika dakika za lala salama liliwezesha United kufikisha pointi sawa na Manchester City ambao wana pointi 47 katika msimamo wa ligi.
 Matokeo ya leo yamezidi kuwatia nguvu United na kuamini sasa wanaweza kupambana na kufanikiwa kumaliza ndani ya nafasi 4 za juu ili kupata nafasi ya kucheza kwenye Champions League.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here