Home Ligi BUNDESLIGA Hawa ni mastaa wa muziki 13 na club soka wanazoshabikia.

Hawa ni mastaa wa muziki 13 na club soka wanazoshabikia.

892
0
SHARE

1

Msanii Rihanna alisafiri hadi Brazil kwenda kuangalia fainali za kombe la dunia na baada ya Ujerumani kushinda aliungana nao kwenye sherehe za kushangilia ubingwa huo. Hili ni moja ya tukio ambalo linaonyesha mastaa wa muziki nao wanahusudu soka sana.

Hii ni list ya mastaa wa muziki na club wanazoshabikia

JAY Z14Jay Z ni shabiki wa Arsenal na aliwahi kuhusishwa na ishu za kutaka kununua hisa za club hii. Ushabiki wake ulianza baada ya kumuona Henry akicheza na kuvutiwa nae, tangu siku hiyo ameonekana mara nyingi akiwa Emirates Stadium akicheki soka.

JENIFFER LOPEZ12Huyu ni shabiki wa Real Madrid na mara nyingi anavaa jezi ya club hiyo. Muingiliano wa lugha nao unachangia yeye kuvutiwa na club hii kubwa. Mwaka 2012 akiwa Spain alipanda jukwaani ku-perform akiwa amevaa jezi ya Real Madrid.

JUSTIN BIEBER8Bieber alivaa jezi ya Everton mara kadhaa akiwa anacheza soka na kupiga nayo picha. Pia alienda kufanya tour ndani ya uwanja wa Stamford Bridge. Zaidi ya hapo pia alipata nafasi ya kufanya mazoezi na wachezaji wa club ya Barcelona. Bieber anatajwa kuwa shabiki wa club 3 ambazo ni Everton, Chelsea na Everton.

DR DRE37Dr Dre anasema ameanza kuipenda Liverpool ikishinda magoli 5 wakati akiwa kwenye tour yake nchini England. Hadi leo ameendelea kuwa shabiki wa club hiyo.

DRAKE1Huyu hamaa ana ugonjwa wa kupenda club nyingi. Lakini urafiki wake na Didier Drogba na Rio Ferdinand umemfanya aendelee kuwa shabiki wa Manchester United na Chelsea. Lakini pia anashabikia Liverpool, Man City na timu ya kwao Toronto FC.

SHAKIRA6Huyu dada aliwai kupewa jezi ya Real Madrid na Zinedine Zidane lakini mambo ya familia yamemzidia. Baada ya kuanza uhusiano wa mapenzi na Gerard Pique amekua shabiki mkubwa wa Barcelona.

ADELE5Amezaliwa Tottenham na amekua akiona familia yake ikishabikia Spurs. Hii ni moja ya sababu kubwa ya yeye kuwa shabiki wa Spurs na anaenda hadi uwanjani.

CHRIS MARTIN23Huyu jamaa alifanya vizuri kwenye ngoma ya Coming Home ya Kanye West ambapo aliimba chorus kali. Yeye ni shabiki Exeter City. Mara nyingi ame-post kwenye social network aki-support club hii ambayo inatoka kwenye mji ambao amezaliwa. Lakini mara kadhaa pia anaonekana kwenye mechi za Arsenal.

ENRIQUE IGLESIAS10Baba ake Enrique alikua kipa kwenye timu ya watoto wa Real Madrid kabla ajali ya gali haijamaliza career yake. Sasa mwanae amebaki kuwa shabiki wa club hii kama baba yake hadi leo.

LUCIANO PABAROTTI9Mkongwe kwenye muziki ni shabiki wa Juventus, mara nyingi alikua anaenda kucheki mechi za Juventus. Hata alivyofariki wachezaji kadhaa wa Juventus walienda kwenye msiba wake mwaka 2007.

LANA DEL REY7Msanii Lana amesema kwamba manager wake ambae ni die hard fan wa Liverpool alimuambia mambo mengi kuhusu club hiyo. Hadi akaanza kuishabikia. Tangu mwaka 2013 ameanza kwenda kwenye uwanja wa Anfield.

 

ELTON JOHN4Huyu jamaa amewai kumiliki hisa za Watford mara mbili. Hadi hivi sasa wanamtambua kama shabiki wa heshima wa club hiyo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here