Home Ligi EPL Danny Welbeck amzungumzia Marcus Rashford

Danny Welbeck amzungumzia Marcus Rashford

730
0
SHARE

cov

Kama hujui njia aliyopitia Rashford na Welbeck hazitofautiani sana. Wote wawili wamepitia academy moja ya watoto ambayo baadae ikawapeleka Manchester United academy na kujiunga na timu ya wakubwa.

Kama ilivyokua kwa Welbeck imekua hivyo hivyo kwa Rashford ambae ameanza kwa kishindo kwenye mechi za EPL. Welbeck aliulizwa kuhusu future ya Rashford anaionaje, “Anafanya vizuri sana, mimi binafsi nilifurahishwa na jinsi anavyocheza na hasa alivyoingia kwa kishindo kwenye EPL kama alivyofanya kwenye Europa League. Nadhani ataendelea kufanya vizuri.”

Rashford alitupia mara mbili kwenye mechi yake ya kwanza Alhamisi kwa kufunga mara mbili kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya FC Midtjylland. Baada ya hapo zikafuatiwa na mbili nyingine kwenye mechi dhidi ya Arsenal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here