Home Kimataifa Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa...

Juve yaponea tundu la Sindano kwa Inter – Penati zawabeba. Fainali sasa vs AC Milan

556
0
SHARE

img_4002.jpg

Aibu nusra iwakumbe wakubwa usiku wa kuamkia leo huko Italia ndani ya Jiji la Milan.

Mabingwa watetezi wa kombe la Coppa Italia Juventus leo wameepuka kuvuliwa ubingwa wao huo baada ya kukubali ushindi wao wa 3-0 katika mechi ya kwanza kule Turin kupinduliwa na vijana wa Roberto Mancini kwa kupigwa 3-0 na Milan ndani ya dakika 90 za mchezo marejeano. Lakini mwishowe bahati ikawa upande kwa kushinda kwa penati 5-3 na kutinga fainali.
 Inter wakiingia kwenye mchezo huo wa nusu fainali ya pili ya Coppa Italia wakiwa na deni la magoli matatu waliyofungaa Turin January 27, walifanikiwa kupambana na kurudisha deni hilo kwa magoli ya Marcelo Brozovic dakika 16, Ivan Perisc akapiga la pili dakika ya 49, kabla ua Brozovic kufunga la 3, na mpaka dakika 90 za kawaida zinamalizika matokeo ya jumla yakawa 3-3, na hivyo mwamuzi akaamuru zichezwe dakika 30 za muda wa ziada.

Hata hivyo katika dakika 30 za nyongeza hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango ka mwenzake na hivyo mechi ikabidi iamuriwe kwa mikwaju ya penati ambayo Juventus wakaibuka na ushindi wa 5-4, beki wa kiargentina wa Milan Rodrigo Palacio akikosa penati na Leornardo Bonucci akafunga penati iliyoamua mechi upande aa Juventus.
Juventus sasa watacheza fainali ya kutetea ubingwa wao tarehe 21 May jijini Rome dhidi ya ACMilan, ambao nao walifanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo kwa kuifunga 5-0 Alessandria juzi Jumanne.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here