Home Kimataifa Taji la ‘Comeback Kings’ sasa lipo mikononi mwa Barcelona 

Taji la ‘Comeback Kings’ sasa lipo mikononi mwa Barcelona 

960
0
SHARE

FC Barcelona wanaongoza ligi kwa pointi 8 mbele ya Atletico Madrid wanaoshika nafasi ya pili na pointi 12 mbele ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid.

  Kikosi cha Luis Enrique pia wapo kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Copa Del Rey, ambapo watacheza dhidi ya Sevilla. Kwa upande mwingine tayari wameshaingiza mguu mmoja kwenye robo fainali ya Champions League kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Arsenal @Emirates.

Mpaka kufikia sasa, msimu wao unaonekana kwenda vizuri kwenda kushinda makombe mengine matatu kama msimu uliopita. Lakini sio kila kitu kilikuwa rahisi kama kinavyoonekana. Kwa mara tisa iliwabidi kutoka nyuma kwa goli na kwenda kushinda mechi. Msimu huu, The Blaugrana wamekuwa the New King of Comebacks.

  Mechi ya kwanza ilikuwa mwezi August. Ilikuwa kwenye European Super Cup, dhidi ya Sevilla. Barça walishinda kombe hilo (Kombe lao la 4 kwa mwaka 2015, La Liga, Copa Del Rey, Champions Legaue), lakini iliwabidi kupambana kurudisha goli la Ever Banega walilofungwa dakika ya pili huko Georgia. Mwishoni mwa mchezo Barca wakashinda 5-4 baada ya muda wa ziada shukrani kwa goli la Pedro ambalo lilikuwa la mwisho akiwa mchezaji wa Barca.

  Mechi iliyofuatia ilikuwa pale Vicente Calderon, mchezo wa 3 wa ligi. Ndio mchezo pekee ambao Barca walitoka nyuma na kwenda kushinda mchezo wakiwa ugenini. Fernando Torres alianza kuifungia Atletico katika kipindi cha pili, lakini Lionel Messi na Neymar wakaisaidia timu yao kubadili matokeo.

  Comebacks nyingine zote zilizofuatia zilikuwa nyumbani kwao Nou Camp. Kwa mara saba kwenye mechi tofauti, mashabiki wa Camp Waliiona timu ikitangulia kwenye ubao wa matokeo. Lakini uwezo wa timu hii ya Barca ulionekana zaidi kwa kuweza kuyabadili matokeo ya mwisho kuwa ya chanya upande wao: Mara nne kwenye La Liga, mara mbili kwenye Copa, na mara moja kwenye Champions League. Mechi ya kwanza pale Camp Nou ilikuwa dhidi ya Bayer Leverkusen, katika hatua ya makundi ya UCl. Magoli mawili ya dakika za mwisho ya Sergi Roberto (80) na Luis Suarez (82) yaliwapa Barca kicheko cha mwisho kwenye mchezo huo baada ya goli la mapema la Papadopoulos’. 
Kwenye La Liga, walifanikiwa kutoka nyuma na kushinda dhidi ya Rayo Vallecano (5-2), Eibar (3-1), Atletico (2-1) Sevilla (2-1).
Kwa upande wa Copa del Rey, waliwafunga Espanyol (4-1) na Athletic Club (3-1) baada ya kukubali kuanza kufungwa mwanzoni.

  MECHI 9 WALIZOANZA KUFUNGWA BARCA NA MWISHONI WAKASHINDA


1.- FC BARCELONA-SEVILLA (5-4).
SUPERCOPA DE EUROPA. 11/8/2015. 0-1, Banega, 2′. 1-1, Messi, 6′. 2-1, Messi, 15′. 3-1, Rafinha, 43′. 4-1, Luis Suárez, 55′. 4-2, Reyes, 60′. 4-3, Gameiro, 73′. 4-4, Nonoplyanka, 84′. 5-4, Pedro, 115′.

2.- ATLÉTICO-FC BARCELONA (1-2). LIGA. Jornada 3. 12/9/2015. 1-0, Torres, 50′. 1-1, Messi, 54′. 1-2, Neymar, 76′.

3.- FC BARCELONA-BAYER LEVERKUSEN
(2-1). CHAMPIONS. Jornada 2. 29/9/2015. 0-1, Papadopoulos, 21′. 1-1, Sergi Roberto, 80′. 2-1, Luis Suárez, 82′.

4.- FC BARCELONA-RAYO VALLECANO (5-2). LIGA. Jornada 8. 17/10/2015. 0-1, Javi Guerra, 14′. 1-1, Neymar, 21′. 2-1, Neymar, 31′. 3-1, Neymar, 67′. 4-1, Neymar, 68′. 5-1, Luis Suárez, 75′. 5-2, Jozabed, 84′.

5.- FC BARCELONA-EIBAR (3-1). LIGA. Jornada 9. 25/10/2015. 0-1, Borja Bastón, 9′. 1-1, Luis Suárez, 20′. 2-1, Luis Suárez, 47′. 3-1, Luis Suárez, 84′.

6.- FC BARCELONA-ESPANYOL (4-1). COPA. Ida 1/8 final. 6/1/2016. 0-1, Caicedo, 8′. 1-1, Messi, 12′. 2-1, Messi, 43′. 3-1, Piqué, 50′. 4-1, Neymar, 89′.

7.- FC BARCELONA-ATHLETIC (3-1). COPA. Vuelta 1/4 final. 27/1/2016. 0-1, Williams, 11′. 1-1, Luis Suárez, 52′. 2-1, Piqué, 80′. 3-1, Neymar, 90′.

8.- FC BARCELONA-ATLÉTICO (2-1). LIGA. Jornada 22. 30/1/2016. 0-1, Koke, 9′. 1-1, Messi, 29′. 2-1, Luis Suárez, 37′.

9.- FC BARCELONA-SEVILLA (2-1). LIGA. Jornada 26. 28/2/2016. 0-1, Vitolo, 19′. 1-1, Messi, 30′. 2-1, Piqué, 46′.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here