Home Ligi EPL Guus Hiddink : LVG analeta Judo uwanjani

Guus Hiddink : LVG analeta Judo uwanjani

607
0
SHARE

d

Baada ya mechi ya Arsenal Vs Manchester United kilicho tend sana sio matokeo peke yake na Rashford, lakini picha ya LVG akijiangusha mbele ya refa wa nje nayo ilisambaa sana.

Hadi sasa imepitia editing nyingi sana kwenye internet ambapo ikihusishwa kwenye vichekesho mbalimbali. Sasa kocha mholanzi mwenzake Guus Hiddink alivyokua kwenye press na waandishi wa habari aliulizwa kuhusu kitendo kile na alimtania kama hivi.

Guus Hiddink,“LVG unaweza kuona jinsi gani analeta Judo uwanjani. Amejidondosha vizuri sana. Mimi nilikua nacheza Judo na kwa jinsi ninavyoona amejidondosha vizuri na mimi naweza kufanya kama vile.”

Kocha wa Chelsea Guus aliwahi kuanzisha kitengo cha Judo akiwa kocha wa PSV kwao Uholanzi. “Nilianzisha kitengo cha Judo na mimi nikiwa mmoja wa wanafunzi kwa lengo la kuleta stamina kwenye team. Simaanishi kwamba wachezaji walete Judo wakiwa uwanjani lakini kuwa imara uwanjani ni muhimu sana ili waweze kutawala mchezo.”

Kwenye Judo kocha Hiddink alianza kuwa na mkanda mweupe ambao ni kwa ajili ya beginners na baadae akaingia wa brown na kuacha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here