Home Kimataifa Gonzalo Higuan akatisha shereke za goli la Fiorentina baada ya sekunde 9.

Gonzalo Higuan akatisha shereke za goli la Fiorentina baada ya sekunde 9.

597
0
SHARE

higun

Jana imechezwa mechi kati ya Napoli Vs Fiorentina ambayo iliishia kwa magoli 1-1. Kwenye msimamo wa ligi Napoli ipo namba mbili na points 58 huku Fiorentina ikiwa namba 4 kwa points 53 baada ya mechi ya jana.

Sasa kitu cha kufurahisha kuhusu mechi hii ni pale ambapo Fiorentina walipotangulia kwa kufunga goli kutoka kwa mchezaji wap Marcos Alonso. Lakini goli hilo lilishangiliwa kwa muda mfupi sana.

Waliporudisha mpira kati kuanza zilipigwa pasi chache sana ndani ya sekunde 9 top scorer wa Serie A Gonzalo Higuan alitupia nyavuni na kukatisha sherehe za mashabiki wa Fiorentina hapo hapo.

Mechi ilienda sare hadi mwisho ambapo ikaisha kwa kutoshana nguvu kwa magoli 1-1. HAsi sasa Higuain anaongoza kwa kufunga kwenye Serie A kwa kutupia mara 25 akifuatiwa na Bacca wa Milan na Dybala wa Juventus wote wana magoli 13.

Goli lenyewe ni hili hapa chini na usikubali kupitwa na show kama hizi kwenye Serie A kupitia king’amuzi cha Startimes

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here