Home Kimataifa SAMATTA: KUFUNGA GOLI LA KWANZA NI CHANGAMOTO KWANGU (Audio)

SAMATTA: KUFUNGA GOLI LA KWANZA NI CHANGAMOTO KWANGU (Audio)

551
0
SHARE

IMG-20160228-WA0019

KRC Genk imefanikiwa kuifunga Club Brugge mabao 3-2, lakini story kubwa ni kumshuhudia Mbwana Ally Samatta akifunga bao la tatu ambalo lilikuwa ni bao lake la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo.

Ulikuwa ni mchezo wake wa nne akitokea benchi leo kwenye mchezo ambao Genk walikuwa wakihitaji pointi tatu muhimu huku wakihitaji kumaliza katika nafasi 6 za juu ili waweze kuingia kwenye play off. wamefanikiwa kupata ushindi huo  na kutengeneza mazingira mazuri ya kuweza kumaliza katika nafasi 6 za juu kwenye ligi.

Baada ya mchezo kumalizika, Mbwana Samatta amezungumzia namna ambavyo amejisikia hasa baada ya kufunga bao la kwanza akiwa na klabu yake mpya ya Genk.

“Ni kitu ambacho nilikuwa nakiota, kila siku unapokuwa kwenye timu mpya watu wanaangalia action yako ya kwanza yaani umeanzaje kwenye timu mpya na ni kitu muhimu kuwa na confidence baada ya hapo inahitaji kuendeleza kwahiyo ndiyo chalenge ambayo imebaki kwangu mimi”, anasema Samatta ambaye ni nahodha wa kikosi cha Taifa Stars.

“Kwasababu kama mwanzo tayari umeshaonekana ni mzuri lakini ngumu ni kuendelea kuwa hivyo nafikiri ni changamoto kwangu na nitajitahidi niweze kushinda hiyo changamoto na niendelee kufunga magoli”.

Shaffihdauda.co.tz: Mechi ilipomalizika ulipata nafasi ya kuongea na kocha na amekwambia kitu gani?

Samatta: Kocha amenipongeza kwasababu ni goli langu la kwanza nadhani kila mmoja alikuwa analisubiri hilo goli ukiacha watanzania ambao walikuwa wakisubiri, lakini karibu wachezaji wote na mashabiki wa klabu pia walikuwa wanasubiri hicho kitu na wamekuwa ni watu wenye furaha sana leo. Wamenipongeza na walikuwa wakiimba ‘Samagoal’ kwahiyo ni furaha kwakweli najisikia vizuri wachezaji wenzangu wananipa support nzuri.

Shaffihdauda.co.tz: Baada ya mechi kuwa imemalizika nilona kama umekuwa mwepesi sana, kwanini ulionekana hivyo?

Samatta: “Kwasababu nahisi kitu ambacho kilikuwa kinaninyima usingizi ni kufunga goli la kwanza, nilikuwa nikipokea comments nyingi kwenye mitandao ya kijamii kwamba watu wanahitaji goli la kwanza wanahitaji kuniona nafanya vizuri kama nilivyokuwa nilipotoka. Ilikuwa inaniumiza na ilinifanya niwe nakifikiria kitu hicho muda wote. Namshukuru Mungu kimefanikiwa leo kwahiyo kilichobaki kwangu ni kuendeleza”.

Pia wachezaji wenzake kwenye klabu ya Genk kama mshambuliaji Nikolaos Karelis  ambaye mara kadhaa amekuwa akianza na Samatta akiingia kuchukua nafasi yake kama ilivyokuwa kwenye mechi dhidi ya Club Brugge alitoka na Samatta kuingia hatimaye kufunga bao la tatu.

Karelis alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati, hapa anamzungumzia Mbwana Samatta baada ya kufunga bao lake la kwanza.

“Ni mchezaji mzuri, amefika hivi karibuni na kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza leo. Anahitaji kuendelea kama hivi nadhani atafanikiwa”, anasema Karelis mara baada ya Samatta kutikisa wavu kwa mara ya kwanza kwenye ligi ya Ubelgiji.

Ukitaka story nzima ingia hapa umsikilize Samatta mwanzo mwisho akielezea furaha yake baada ya kupachika bao la kwanza akiwa Genk.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here