Home Entertainment JB AMEPOST UJUMBE MZITO INSTAGRAM AKIMKUMBUKA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA

JB AMEPOST UJUMBE MZITO INSTAGRAM AKIMKUMBUKA MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA

712
0
SHARE
Superstar mwingine wa Bongo Movies JB akiwa nje ya uwanja muda mfupi kabla ya pambano la Yanga vs Simba halijaanza, JB ni mnazi mkubwa wa mnyama wa Msimbazi

Superstar mwingine wa Bongo Movies JB akiwa nje ya uwanja muda mfupi kabla ya pambano la Yanga vs Simba halijaanza, JB ni mnazi mkubwa wa mnyama wa Msimbazi

Msanii maarufu kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Movies Jacob Steven ‘JB’ leo amepost ujumbe kwenye account yake ya instagram akimkumbuka mchezaji wa zamani wa Simba Edward Chumira ambaye alifariki tarehe kama ya leo mika 15 iliyopita.

JB ni shabiki mkubwa wa mnyama na amekuwa akihudhuria mara kadhaa kuishuhudia timu hiyo inapokuwa uwanjani kukipiga mechi mbalimbali hasa za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

JB 2

Gwiji huyo amepost ujumbe unaosomeka hivi: “Mwaka 2001 tarehe kama ya leo wapenda mpira wote walikuwa na majonzi baada ya mshambuliaji wa Simba Edward Chumira Eddo boy kufariki. Ni miaka 15 sasa, unakumbukwa na wanasimba wenzako, dada yako ambaye pia ni msanii mwenzetu Herieth Chumirana mwanao”.

“Binafsi nakumbuka ulivyokuwa unacheza na pacha mwenzako fundi Matola Soma. Pumzika kwa amani brother Edward Chumira”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here