Home Kimataifa Hatimaye PSG wasimamishwa Ligue 1 – Washindwa kuifikia rekodi ya Nantes 

Hatimaye PSG wasimamishwa Ligue 1 – Washindwa kuifikia rekodi ya Nantes 

697
0
SHARE

Waingereza wana msemo wao unaosema – (‘All the goods things come to an end’ – ‘Kila Jambo zuri hufikia mwishoni.’

  Msemo huu unaendana na kilichotokea usiku wa tarehe 28/2/2016 – Lyon waliwashangaza Paris Saint-Germain kwa kipigo cha 2-1 na kusitisha safari ya mabingwa watetezi kumaliza ligi bila kufungwa.

  Kinda wa Lyon Maxwell Cornet aliwapa uongozi wa mechi vijana wa Bruno Genesio mwanzoni mwa mchezo kabla ya Segie Darder kuongeza la pili na kuipeleka Lyon mapumziko wakiwa mbele 2-0.

  Lucas Moura alifanikiwa kurudisha goli moja lakini Lyon walikaza na kufanikiwa kupata ushindi ambao uliwaingiza kwenye Top 3 ya Ligue 1.

Matokeo hayo yamehitimisha rekodi ya PSG kutokufungwa katika mechi 36 katika Ligue 1 – rekodi iliyoanzia msimu uliopita, mechi yao ya mwisho kufungwa ilikuwa dhidi ya Bordeaux – walipofungwa 3-2.

  Rekodi ya kucheza mechi nyingi bila kufungwa kwenye Ligue 1 ndani ya msimu inashikwa na Nantes, mechi 32, rekodi hii waliweka msimu wa 1995/95. PSG wameishia mechi 27 bila kupoteza msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here