Home Kimataifa YAJUE MAMBO 10 KUHUSU JIWE LA VETO LA NCHINI ARGENTINA

YAJUE MAMBO 10 KUHUSU JIWE LA VETO LA NCHINI ARGENTINA

747
0
SHARE

Paulo Dybala 1

Na Athumani Adam

Taifa la Argentina limejaliwa kuwa na vipaji vingi vya soka, lakini kwenye nafasi ya ushambuliaji  wanatisha zaidi. Wanatisha kuanzia enzi za Diego Maradano, Gabriel Batistuta hadi leo hii Sergio Aguero, Lionel Messi, Gonzalo Higuin bado wanaendelea kufanya vizuri.

Makala hii inakuletea mambo kumi (10) kuhusu mshambuliaji chipukizi anayetisha na Juvevuntus kwa sasa kwenye ligi ya Italia Serie A,  raia wa Argentina Paulo Dybala.

Paulo Dybala

  • Anaitwa Paulo Bruno Exequiel Dybala, alizaliwa 15 November 1993 huko Cordoba nchini Argentina. Babu yake mzee Boleslaw Dybala ana asili ya Poland na bibi yake ana asili ya Italia.
  • Akiwa na timu ya Cordoba kwenye ligi daraja la pili nchini Argentina maarufu kama Primera B Nacional, Dybala alipewa jina la utani La Joya. La Joya ni neno la kihispania lenye maana ya veto (jewel). Alipewa jina hilo kwasababu ya uwezo wake mkubwa.
  • Akiwa na umri wa miaka 17, alivunja rekodi ya gwiji wa zamani wa Argentina mfungaji bora na mchezaji bora wa kombe la dunia 1978, Mario Kempes. Dybala alivunja rekodi na kuwa mchezaji mdogo kabisa kufunga goli kwenye ligi ya kulipwa ndani ya Argentina akiwa na Cordoba. Pia alifunga magoli 17 kwenye mechi 40.
  • Akiwa na Cordoba, alifanikiwa kufunga hat-trick mbili kwenye msimu mmoja, pia alivunja tena rekodi ya gwiji wa zamani wa Argentina mshindi mara mbili wa tuzo ya pichichi akiwa na Valencia Mario Kempes. Dybala alivunja rekodi ya kucheza mechi nyingi mfululizo ndani ya msimu, alicheza mechi 38 za Primera B Nacional.
  • Raisi wa Palermo, Maurizio Zamparini aliwahi kumfananisha Dybala na Sergio Aguero wakati aliposajiliwa kutoka Cordoba kwenda Palermo April 2012.
  • Alifanikiwa kufunga goli lake la kwanza na pili akiwa ndani ya Italia pale Palermo walipoilaza Sampdoria 2-0 nyumbani.
  • Alipewa jezi namba 21 ya mkongwe Andrea Pirlo baada ya kusajiliwa kutoka Palermo June mwaka 2015 kwa dau la Euro million 32. Alihamia Juve baada ya kufunga magoli kumi nusu ya msimu mwaka 2014-2015, alimaliza msimu akiwa na goli 13 na pasi za mwisho 10.
  • Alifunga goli la kwanza kwenye serie A, akiwa na Juve August 2015 kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya As Roma.
  • Angeweza kuchezea timu za taifa za Poland na Italy, Dybala alichagua kuchezea taifa la Argentina. Aliitwa mara ya kwanza kwenye timu ya wakubwa ya Argentina September 22, 2015 na kocha Gerardo Martino.
  • Mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Argentina ilikuwa 13 october 2015. Aliingia dakika ya 75 kuchukua nafasi ya Tevez kwenye mechi ya kufuzu kombe la dunia 2018 dhidi ya Paraguay.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here