Home Kimataifa KUTOKA ZURICH: SHAFFIH DAUDA NA UCHAMBUZI WA UCHAGUZI WA FIFA

KUTOKA ZURICH: SHAFFIH DAUDA NA UCHAMBUZI WA UCHAGUZI WA FIFA

545
0
SHARE

IMG-20160226-WA0015

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limepata rais mpya Gianni Infantino ambaye atakaa madarakani hadi mwaka 2019 kuongoza chama hicho kinachosimamia mchezo wa soka duniani.

Shaffih Dauda alikuwe Zurich, Swiss kushdia zoezi hilo linavyoendelea na anakuletea uchambuzi ufuatao jinsi na namna zoezi hilo lilivyoendeshwa hadi kumpata rais huyo mpya atakae simamia soka la ulimwengu.

Wajumbe wameyapokeaje matokeo ya ushindi wa Gianni Infantino?

Mgombea kutoka vyama za soka barani Ulaya UEFA amefanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha urais wa FIFA mwaka 2016 na atakaa madarakani hadi mwaka 2019. Wajumbe wamepokea matokeao vizuri kwasababu mchakato wa uchaguzi umekwenda salama kabisa kwa kuzingatia demokrasia ya hali ya juu. Wagombea walifanya campaign katika kipindi ambacho walitakiwa kufanya hivyo na campaign ziliwavutia wajumbe wengi kwasababu wagombea wote walikuwa wanasisitiza kurejesha umoja ndani ya FIFA.

Kitu kingine  kilichosisitizwa na wagombea hao kilikuwa ni kusafisha taswira ya shirikisho hilo la mchezo wa soka na Gianni Infantino mwisho wasiku akawa ameshinda na kuwa rais mpya wa FIFA  kitu ambacho kimefurahiwa na wajumbe ambao walikuwepo kuhakikisha mshindi anapatikana.

Mazingira ya upigaji kura na demokrasia vilizingatiwa?

Mazingira ya upigaji kura yalikuwa ya kidemokrasia zaidi baada ya kutoka tamko la kuwazuia wapiga kura kwenda na simu zao pamoja na camera kwenye chumba cha kupigia kura. Ilionekana inajenga mazingira ya kidemokrasia kwa wagombea wa nafasi ya kiti cha urais wa FIFA na namna ambavyo wapigakura walivyokuwa wanakwenda kupiga kura pasipo kupoteza muda zoezi ambalo lilikuwa ni la wazi.

Uchaguzi huo ulikuwa unaoneshwa moja kwa moja kupitia youtube channel ya FIFA TV na television nyingine duniani ambazo zilikuwa na haki ya kuonesha tukio hilo namna ambavyo kura zilikuwa zikipigwa kwa uwazi huku demokrasia ikiwa imezingatiwa kwa kiwango cha juu.

Upinzani kati ya wagombea wa kiti hicho ulikuwaje?

Awali upepo ulikuwa unamwangazia Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa na hiyo ni kutokana na support ambayo alikuwa anaipata moja kwa moja kutoka Afrika ikumbukwe bara la Afrika linawajumbe wengi sana wanaopiga kura kwenye mkutano mkuu wa FIFA pia yeye alikuwa akitoka bara la Asia ambalo lina kura 47 na tayari mataifa zaidi ya 31 yalishaonesha nia ya dhati ya kumsupport kutoka bara la Asia.

IMG-20160226-WA0014

Yeye akiwa rais wa chama cha soka cha Asia ukijumlisha na kura 54 ambazo zinatoka bara la Afrika ilikuwa inaonekana kwa kiasi kikubwa Sheikh Salman angeweza kupata 2/3 ya kura katika duru la kwanza. Hata kama ingeshindikana basi angeweza kupata kura katika duru la pili ambalo wanazungumzia simple majority kwa maana ya mshindi kupata zaidi ya nusu ya kura zote.

Lakini ilikuwa ni tofauti na matarajio ya namna ilivyokuwa hapo awali baada ya duru la kwanza kumalizika kwa Gianni Infantino kupata kura 88 akimzidi pointi tatu Sheikh Salman aliyekuwa amepata kura 85 wakati Prince Ali akiwa amepata kura 27.

Lilipoingia duru la pili ilionekana dhahiri shahiri upinzani uliokuwepo kati ya Sheikh Salman pamoja na Prince Ali ulikuwa unamuangamiza Sheikh Salman kwasababu ilionekana zile kura 27 za Prince Ali zingehamia kwa Gianni Infantino na ndicho kilichotokea.

Duru la pili Gianni Infantino akapata kura 115 huku Sheikh Salman akipata kura 3 zaidi ya alizopta mwazo yaani kura 88. Gianni Infantino akatangazwa rais wa FIFA kwa kushinda zaidi ya nusu ya kura ambazo zilikuwa zinatakiwa kuwa 104 tu katika duru hilo la pili.

Baada ya uchaguliwa Gianni Infantino anasemaje?

Baada ya kuchaguliwa, Gianni Infantino amesisitiza umoja kurejea na kuvunja makundi yote yaliyokuwepo wakati wa mchakato wa uchaguzi.

Lakini kikubwa alichokisema wakati wa campaign alizungumzia namna ya kuongeza vyanzo vya mapato kwa kupitia fedha za FIFA akisisitiza fedha za FIFA  ni fedha za za vyama 209 na si pesa za shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.

Akasema akifanikiwa kuingia madarakani atatafuta namna ya kuongeza vyanzo vya mapato kutokana na pesa za FIFA lengo likiwa ni kuongeza pesa kwa vyama wanachama ambazo zitawasaidia kutekeleza program mbalimbali za maendeleo ya soka kwenye nchi zao.

Amesema pia atazunguka dunia nzima kuhakikisha anaona namna maendeleo ya soka yanavyoendelea katika hivyo vyama vya soka 209 ulimwenguni kote.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here