Home Kitaifa JKT RUVU YATEMA RASMI TAJI, COASTAL YATINGA ROBO FAINALI, ‘MBEYA DERBY’ KUNOGESHA...

JKT RUVU YATEMA RASMI TAJI, COASTAL YATINGA ROBO FAINALI, ‘MBEYA DERBY’ KUNOGESHA FA CUP LEO

549
0
SHARE
Mussa Juma (kulia) wa JKT Ruvu akichuana kuwania mpira na Yusuph Chuma wa Coastal Union
Mussa Juma (kulia) wa JKT Ruvu akichuana kuwania mpira na Yusuph Chuma wa Coastal Union
Mussa Juma (kulia) wa JKT Ruvu akichuana kuwania mpira na Yusuph Chuma wa Coastal Union wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara (VPL) uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Karume, Dar

Na Baraka Mbolembole

Mabingwa watetezi wa kombe la FA timu ya JKT Ruvu ya Pwani ‘imeutema’ rasmi ubingwa wa michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha magoli 3-0 mbele ya Ndanda SC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara siku ya Ijumaa (jana).

Magoli ya wenyeji yalifungwa sasa timu hiyo changa katika mpira wa Tanzania imefanikiwa kufika hatua ya robo fainali ikiungana na timu ya Yanga SC iliyoitoa JKT Mlale ya Ruvuma siku ya Jumatano iliyopita.

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara, Coastal Union ya Tanga licha ya kukabiliwa na matatizo mengi ya kifedha hadi kufikia wachezaji wa timu hiyo kuandamana siku ya Alhamisi wakishinikiza kulipwa kwa stahiki zao za mishahara ya miezi takribani mitatu sasa.

Wachezaji ambao waliahidi kuendelea kufanya kazi yao uwanjani kabla ya mchezo wao wa jana Ijumaa dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Katika timu kongwe zinazocheza mpira Mtibwa ni mojawapo kati ya timu zinazotisha, kuwafunga 1-0 nimefarijika sana ingawa bado nina-uchungu kwa sababu katika msimamo wa ligi hatupo katika nafasi nzuri”, anasema kocha mkuu wa Coastal, Ally Jangalu mara baada ya timu yake  kuifunga Mtibwa na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya FA.

Michuano hiyo itaendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa katika miji tofauti. Jijini, Mbeya, mahasimu wa jiji hilo Mbeya City FC itawavaa Tanzania Prisons katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali leo Jumamosi. Huko mkoani Shinyanga, wenyeji Mwadui FC watawavaa Rhino Rangers ya Tabora katika uwanja wa Mwadui Complex.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here