Home Dauda TV HIKI NDICHO ALICHOFANYA MESSI BAADA YA KUVUNJA REKODI YA CECH (Video)

HIKI NDICHO ALICHOFANYA MESSI BAADA YA KUVUNJA REKODI YA CECH (Video)

504
0
SHARE

Messi vs Cech

Leo Messi hatimaye alifuta ukame wa magoli dhidi ya Petr Cech siku ya Jumanne usiku, mu-Argentina huyo alikuwa hajafunga goli lolote dhidi ya golikipa huyo raia wa Czech.

Messi alikuwa amekutanana Cech kwenye michezo sita nyuma (wakati Cech alipokuwa akicheza kwenye klabu ya Chelsea) lakini alishindwa kufunga goli kwa zaidi ya saa 10 ukijumlisha dakika ambazo Messi alicheza kwenye michezo yote waliyokutana.

Na hiyo ikazaa dhana kwamba, Cech alikuwa anauwezo wa kuzuia michomo ya Messi, lakini nyota huyo wa Barcelona akafanikiwa kuvunja mwiko huo kwa kutupia bao mbili kwenye uwanja wa Emirates.

Kuonesha kwamba hakuna uhasama kati yao, wawili hao walikumbatina baada ya mchezo huo kama video inavyoonesha hapa chini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here