Home Ligi EPL Marcus Rashford: Shujaa Mpya Old Trafford Aliyevunja Rekodi ya George Best

Marcus Rashford: Shujaa Mpya Old Trafford Aliyevunja Rekodi ya George Best

2407
0
SHARE

Marcus Rashford alikuwa shujaa ambaye hakutabiriwa usiku wa Alhamisi dhidi ya FC Midtjylland, akifunga magoli mawili katika mechi yake ya kwanza ya kikosi cha kwanza katika ushindi wa 5-1 ambao uliiwezesha United kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-3 na sasa wanaelekea hatua ya 16 bora ya Europa League.

  Magoli hayo yalikuja wakati muhimu – na kuipa United uongozi wa 2-1 na kisha 3-1 na kubadili kabisa hali ya mchezo. Rushford alianza mchezo huo baada ya Anthony Martial kuumia wakati akipasha misuli – kabla ya usiku wa Alhamisi alikuwa hafahamiki, nje ya Manchester.
Hivi ndio vitu 5 kuhusiana na shujaa mpya wa Old Trafford.

1. Asili Yake
Rashford alizaliwa jijini Manchester mnamo mwaka 1997 na aliwahi kuitumikia Fletcher Moss Junior club, klabu ambayo iliwatengeneza akina Wes Brown, Danny Welbeck na wengine kama Tyler Blackett na Cameron Borthwick-Jackson. Rashford alijiunga na United na ametokea kwenye akademmi za Man United na kufanikiwa kuwakosha walimu wake.

   
 2. Uongozi
Mashindano ya UEFA Youth League ndio ambayo aliweza kung’ara sana msimu huu, akifunga mara mbili dhidi ya PSV Eindhoven na dhidi ya Wolfsburg. Kocha wa timu ya vijana Nicky Butt, kiungo wa zamani wa United, alimpa unahodha.

  3. Uaminifu
Kulikuwepo na ushawishi wa kujiunga na Manchester City kwa Rashford msimu uliopita lakini akaamua kubaki na kuendelea kujifunza. Goli la kwanza la mshambuliaji huyo lilikuja akitokea benchi katika mechi ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Leicester mwezi December 2015.

  4. Uzoefu
Rashford alikiwa katika benchi la kikosi cha kwanza cha United kwenye Premier League katika mechi mbili dhidi ya Watford na Leceister mwishoni mwa November. Zote zilikuwa mechi za ugenini na moja walishinda vs Watford (2-1) na nyingine walitoka sare ya 1-1 na Leceister lakini Rashford hakucheza kabisa.

  5. Utamaduni
Rashford bado ana miaka 18 na anajiunga na listi ya wachezaji chipukizi ambao waliifungia United, Wayne Rooney Federico Macheda, Adnan Januzaj lakini Rashford ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi (Miaka 18 na siku 117) wa United katika michuano ya ulaya – akiivunja rekodi ya George Best – Rashford pia amefunga magoli katika vikosi vya U18, U19, U21 na sasa kikosi cha kwanza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here