Home Kimataifa JONESIA RUKYAA SI MWAMUZI WA KWANZA MWANAMKE, HII NDIYO TOP 10 YA...

JONESIA RUKYAA SI MWAMUZI WA KWANZA MWANAMKE, HII NDIYO TOP 10 YA MAREFA BORA WA KIKE DUNIANI

1075
0
SHARE

ref 3

Katika soka refarii anakuwa na nafasi kubwa sana ya kuufanya mchezo wa soka kuwa mzuri au kuuharibu. Katika soka refarii anakuwa na kazi ya kusimamia sheria za mchezo wa soka na kama muamuzi wa mwisho katika mechi refarii ndio ana uwezo wa kuamuru pambano liendelee au lisiendelee.

Jumamosi iliyopita mwamuzi wa kikek wa kitanzania Jonesia Rukyaa alichezesha pambano la watani wa jadi Yanga vs Simba lililomalizika kwa Yanga kushinda kwa bao 2-0.

Moja ya matukio yanayokubukwa kwenye mchezo huo ni pamoja na mwanadada huyo kumtoa nje kwa kadi nyekundu beki wa kati wa Simba Abdi Banda baada ya kumwonesha kadi mbili za njano kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Shaffihdauda.co. tz imekuandalia top 10 ya marefarii bora wa kike katika mchezo wa soka na maamuzi ya kukumbukwa waliyowahi kufanya katika baadhi ya mechi muhimu.

  1. Wendy Toms

ref

Refa wa zamani wa ligi kuu ya uingereza ni Muingereza aliyezaliwa 16 october 1962 huko Broadstone Dorset alikuwa refarii wa kwanzawa kike kuamua katika ligi kuu ya Uingereza kama muamuzi wa pembeni. Wendy pia alichaguliwa kama mwamuzi wa kike wa kwanza kuamua ligi ya mpira wa miguu mwaka 1994-1995. Wendy pia alibahatika kuwa mwamuzi wa kike wa kwanza kuamua mechi za Ligi kuu ya Uingereza mwaka 1998-1999, aliamua pia mechi ya Ligi ya mabingwa ulaya ya wanawake hatua ya robo fainali tarehe 30 October 2003 na 2005.

  1. Amy Fearn

ref 1

Muingereza Amy Elizabeth Fearn alizaliwatarehe 20 Novemba mwaka 1977 pale Loughborough Leicestershire na kuwa mwanamke wa kwanza kuamua katika mpira wa miguu mwaka 2010 alianza kujifunza urefarii akiwa na umri wa miaka 14. Amy alifanikiwa kuwa mwamuzi wa kike wa kwanza kuamua mechi kama refarii wa kati tarehe 9 Februari mwaka 2010. Alikuw refarii wa kike wa kwanza katika mchezo wa Kombe la FA mwaka 2013

  1. Bibiana Steinhaus

ref 2

Refarii wa kike kutoka Ujerumani alizaliwa tarehe 24 March mwaka 1979 huko Lauterberg na alikuwa Refarii wa kwanza wa kike katika ligi ya kulipwa ya Nchini Ujerumani alifanikiwa kuwa muamuzi katika mchezo wa mpira wa miguu wa wanawake Bundesliga mwaka 1999. Steinhaus aliamua pambano la wanawake la fainali ya kombe la DFB-Pokal kati ya FFC Frankfurt na FCR 2001 Duisburg mwaka msimu wa 2002-2003. Alichaguliwa pia na FIFA Kuchezesha mashindano ya Kombe la Dunia la wanawake mwaka 2008. Euro ya wanawake mwaka 2009 na kombe la dunia la wanawake chini ya miaka 20 mwaka 2010.

  1. Kari Seitz

ref 3Amezaliwa Marekani tarehe 2 November mwaka 1970 na anachukuliwa kama moja ya waamuzi bora wa kike wa muda wote, aliteuliwa kama muamuzi katika mashindano ya soka ya Olympic mwaka 2004 kule Athens Ugiriki, 2008 Olympic ya Beijing China na mwaka 2012 pale London Uingereza na mashindano ya Kombe la Dunia la wanawake mwaka 1999,2003, 2007 na 2011 na kuiwa mwamuzi wa kike pekee kufikia mafanikio hayo, amekuwa muamuzi kwa miaka 28 ikijumuisha miaka 14 ya soka la kulipwa ambapo Seitz alikaliliwa akisema kuwa ” Kwa upande mwingine ilikuwa ni uamuzi lakini upande mwingine ulikuwa ni wito” kwa yeye kuwa muamuzi wa mchezo wa soka.

  1. Sian Massey-Ellis

ref 4

Ni refarii wa kike Raia wa Uingereza ambaye mpaka sasa ni muamuzi katika ligi kuuu ya Uingereza alizaliwa October mwaka 1985. Amechezesha mikchezo mbalimbali ya kombe la ligi ya mpira wa miguu pamoja na Ligi ya mabingwa Ulaya kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kushiriki mashindano ya kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa wanawake. Alifanikiwa kuwa muamuzi wa mezani katika pambano la kufuzu fainali za kombe la Dunia kati ya Uingereza na Austria tarehe 20 April mwaka 2006. Sian pia amefanikiwa kuamua michezo ya kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa wanawake mwaka 2011

  1. Jacqui Melksham

ref 5

Refarii wa Kike kutoka Autralia alizaliwa tarehe 12 October 1978 huko Australia na anachukuliwa kama moja ya Marefarii bora wa kike. Jacqui aliamua mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Canada mwaka 2011 katika uwanja wa Olympic Berlin Ujerumani tarehe 26 Juni mwaka 2011. Alichaguliwa tena kuwa muamuzi katika pambano la robo fainali kati ya Brazil na Marekani katika uwanja wa Rudolf-Harbig  pale Dresden tarehe 10 Julai mwaka 2011

  1. Sanda Hunt

ref 6

Refarii wa Zamani kutoka Marekani ambaye alizaliwa tarehe 14 June mwaka 1959 na kuwa muamuzi kati ya miaka ya 1996-2004. alifanya kazi kam,a muamuzi wa mezani katika fainali za FIFA za Kombe la dunia la Wanawake mwaka mara mbili mwaka 1999 na mwaka 2003 na alifanikiwa kuamua michezo kadhaa katika mashindano ya Olympic Sydney mwaka 2000.kwa sasa Sandra anaishi Bellingham Washington Marekani ambapo anafanya kazi ya ukocha wa marefarii wa kike.

  1. Jenny Palmqvist

ref 7

Raia wa Sweden aliyezaliwa Korea Kusini alizaliwa tarehe 2 Novemba mwaka 1969 na alikuwa muamuzi kwa michezo mbalimbali ya wanawake ndani na nje ya nchi alifanikiwa kuamua fainali ya mashindano ya Olympic na Fainali za Klabu bingwa barani Ulaya mara mbiuli kati ya miaka ya 2009 na 2012 amewahi kuonesha kadi nyekundu mara moja tu kwa mchezaji wa Korea kaskazini Choe Mi-gyong katika mechi kati ya Korea kaskazini na Marekani katika mashindano ya Olympic ya kiangazi mwaka 2012.

9.Dagma Damkova

ref 8

Mwamuzi wa Mpira wa mioguu raia wa Jamhuri ya Czech alizaliwa tarehe 29 Desemba mwaka 1974 na aliorodhoshwa kama reafrii wa kimataifa mnamo mwaka 1999. Alianza kuchezesha mechi yake ya kwanza kati ya Belarus na Moldova tarehe 17 April mwaka 1999. Alifanikiwa kuwa muamuzi katika fainali ya Olympic mwaka 2008 na Mashindano ya Euro kwa wanawake mwaka 2009 lakini pia alifanikiwa kuwa muamuzi katika Fainali ya Ligi ya mabingwa ulaya wanawake mwaka 2011.Alifanikiwa pia kuwa muamuzi wa mezani katika fainali za kombe la Dunia kwa wanawake  zilizofanyika Nchini China mwaka 2007.

  1. Kirsi Heikkinen

ref 9

Kirsi Heikkinen alizaliwa tarehe 26 Septemba mwaka 1978 na yeye pia anatajwa kuwa moja ya waamuzi  bora wa kike kuwahi kutokea katiuka mchezo huo. amekuwa muamuzi wa mezani kwa mechi nyingi za kimataifa yakiwepo mashindano ya Ulaya mwaka 2009,kombe la Dunia mwaka 2011 pamoja na yale mashindano ya Olympic mwaka 2012 pia alikuwa Refarii katika mashindano ya kombe la dunia wachezaji chini ya umri wa miaka 17 pamoja na kombe la Algarve mwaka 2010. Lakini pia alifanikiwa kuwa muamuzi katika pambano la fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2010.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here