Home Ligi EPL Baada ya Gunners na Chelsea Kunyooshwa – Man City yaitoa kifua mbele...

Baada ya Gunners na Chelsea Kunyooshwa – Man City yaitoa kifua mbele EPL

438
0
SHARE

Baada ya Arsenal na Chelsea  kutopata matokeo mazuri katika mechi za kwanza za hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu bingwa ya ulaya, hatimaye usiku wa usiku wa February 24 klabu ya Man City imeitoa kimasomaso EPL. 

 City ambayo ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Dynamo Kyiv, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.

Magoli ya City yalifungwa kuanzia dakika ya 15 kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero, dakika ya 40 David Silva akapachika goli la pili, kipindi cha pili Dynamo Kyiv walirudi na kusawazisha goli moja kupitia Vitaly Buyalsky dakika ya 58, Yaya Toure akashindilia msumari wa mwisho dakika ya 90. 

  
 Kwa upande mwingine Atletico Madrid walitoka sare ya 0-0 na PSV.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here