Home Ligi EPL KUELEKEA ARSENAL VS BARCELONA, SANCHEZ AUFUNGUA MOYO WAKE KUHUSU BARCA

KUELEKEA ARSENAL VS BARCELONA, SANCHEZ AUFUNGUA MOYO WAKE KUHUSU BARCA

654
0
SHARE

Alexis Sanchez-Barca

Sanchez raia wa Chile atawakabili Barca kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka klabuni hapo na kujiunga na Arsenal ‘The Gunners’ lakini anaamini uamuzi wake wa kuondoka Nou Camp ulikuwa ni sahihi kabisa

Arsenal wanawakaribisha Barcelona katika pambano la kwanza la raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na itakuwa ni mara ya kwanza kwa Sanchez kukutana na klabu yake ya zamani FC Barcelona tangu alipoondoka Nou Camp  Julai mwaka 201.

Winga huyo aliyeshinda kombe la Liga pamoja na Copa Del Rey akiwa na Barcelona amefanikiwa kuifungia Arsenal Magoli 35 mpaka sasa na kunyenyua kombe la FA mwaka jana.

Sanchez anasema hajutii uamuzi wake wa kuihama Barcelona na kujiunga na Arsenal mwaka 2014.

“Sijawahi kujutia uamuzi wangu. Sanchez aliliambia Sunday Mirror. Ilikuwa rahisi kuihama Barcelona

” Nilitrimiza ndoto zangu nilipoelekea pale. Kucheza Spain pamoja na Ligi ya mabingwa. Lakini ni wachezaji wachache sana wanaoweza kucheza kwenye klabu moja kwa muda wao wote wa maisha yao. Kuhama ni kawaida.

Nilitaka kazi mpya  na ujuzi mpya na kwa washambuliaji wengi waliopo Barcelona, ulikuwa ni uamuzi sahihi kuondoka.

Nadhani ulikuwa ni uamuzi sahihi kuondoka na kujiunga na Arsenal na ulikuwa ni uhamisho mzuri. Nafurahia maisha hapa Arsenal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here