Home Dauda TV HIVI NDIVYO FORLAN ANAVYOISHA NA UTAMU WAKE (Video)

HIVI NDIVYO FORLAN ANAVYOISHA NA UTAMU WAKE (Video)

704
0
SHARE

Forlan

Katika umri wa miaka 36, Diego Forlan anauthibitishia ulimwengu kwamba yeye bado ni mshambuliaji wa kiwango cha juu baada ya kuonesha kiwango cha juu wakati akiichezea timu yake ya Penaroldhidi ya Defensor Sporting siku ya Jumapili February 21.

Forlan amekuwa hasisi kwenye vyombo vya habari tangu alipoihama Atletico Madrid na kujiunga na Internacional (Brazil), Cerezo Osaka (Japan) na sasa ameamua kurudi kwenye ligi ya nyumbani kwao Uruguay ambapo anakipiga kwenye klabu ya Penarol.

Penarol illicha Defensor Sporting  kwa bao 5-1huku Forlan akihusika katika kila bao lililofungwa na timu yake katika mchezo huo.

Forlan alifunga bao tatu (hat-trick) kwenye mchezo huo akipiga bao mbili kwa kutumia miguu yote kisha bao la tatu akafunga kwa kichwa hii inaitwa perfect hat-trick.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United alipika bao mbili ambazo zilifungwa na Miguel Murillo.

Angalia video za magoli hayo na kiwango kilichooneshwa na Forlan kwenye mchezo huo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here