Home Kimataifa BWANA MDOGO AVUNJA REKODI YA THIERRY HENRY ILIYODUMU KWA MIAKA 21

BWANA MDOGO AVUNJA REKODI YA THIERRY HENRY ILIYODUMU KWA MIAKA 21

652
0
SHARE

Henry

Bwana mdogo Kylian Mbappe amevunja rekodi ya Thierry Henry iliyodumu kwa miaka 21 ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufunga goli akiwa na timu ya wakubwa ya Monaco inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Kinda huyo ambaye tayari yupo kwenye radar za Liverpool alifunga goli lake la kwanza kwenye kikosi cha wakubwa (senior team) cha Monaco akiwa na umri wa miaka 17.

Kylian Mbappe

Henry aliweka rekodi hiyo mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 17 alipoifungia Monaco goli lake la kwanza lakini Mbappe ameivunja rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 17 lakini akitofautiana miezi na Henry wakati alipoweka rekodi hiyo.

Na rekodi hiyo ianasemekana huenda ikadumu kwa miaka zaidi ya 21 ambayo rekodi ya Henry ilidumu kwa muda tangu alipofunga bao lake la kwanza akiwa kinda wa Monaco mwaka 1995.

Mbappe alifunga goli wakati Monaco inacheza mchezo wake wa ligi ya Ufaransa (Ligue 1) na kuibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Troyes.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here