Home Kimataifa Matokeo ya FA Cup – Na Ratiba ya Hatua Raundi ya 6 

Matokeo ya FA Cup – Na Ratiba ya Hatua Raundi ya 6 

804
0
SHARE

Safari ya Guus Hiddink kuiongoza Chelsea kwa mara ya pili kutwaa kombe la FA Cup inazidi kupata mwanga baada ya jioni ya leo kuiadhibu Manchester City iliyochezesha makinda wengi katika kikosi cha kwanza kwa magoli 5-1.

  Magoli ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa, Willian, Gary Cahill, Eden Hazard and Bertrand Traore – na kupelekea Chelsea kuvuka kwenda hatua ya raundi ya 6 ya michuano hii mikongwe zaidi England.

Kwa upande mwingine Spurs walikubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Crystal Palace, wakati West Ham wakiiadhibu 5-1 Blackburn. Jana Arsenal walicheza na Hull City na kutoka sare ya 0-0.

Manchester United kesho itasafiri kwenda kuumana na Shrewbury na kulingana na ratiba ya FA Cup Raundi ya 6, mshindi wa mechi atakutana na West Ham. 

 
Guus Hiddink atakutana na timu ambayo aliifunga katika fainali ya FA Cup alipokuwa kocha wa muda wa Chelsea mnamo mwaka 2009 – Everton na mechi itapigwa Goodison Park. 

 
Arsenal wakifanikiwa kuitoa Hull City katika mchezo wa marejeano watacheza dhidi ya klabu ya Watford.  

 
Huku wababe wa  Tottenham, vijana wa Allan Pardew wakipangiwa kucheza dhidi ya Reading  

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here