Home Ligi EPL Video: Jose Mourinho Anaenda Manchester, athibitisha Mkurugenzi wa Inter baada ya kukutana...

Video: Jose Mourinho Anaenda Manchester, athibitisha Mkurugenzi wa Inter baada ya kukutana nae

694
0
SHARE

Wakati tetesi za kutimuliwa kwa kocha Louis Van Gaal zikizidi kuongezeka, mmoja wa makocha wanaotajwa kuwa katika listi ya kumrithi Jose Mourinho ameripotiwa kutaja timu atakayoenda kufundisha hivi karibuni. 

  
Kwa mujibu rafiki wa karibu wa kocha huyo wa kireno, mkurugenzi wa klabu ya Inter Milan, Bedy Moratti, amesema kwamba Mourinho atakuwa kocha mpya wa Manchester United. 

Mourinho leo alikutana na Raisi wa klabu ya Inter Milan Massimo Moratti kwa ajili ya chakula cha mchana jijini Milan, Italia, na katika mkutano huo dada yake Raisi wa klabu hiyo ya zamani ya Mourinho, Bedy Moratti pia alihudhuria.

Wakati akiwa anatoka katika mgahawa walipokutana na Mourinho – Bedy Moratti aliulizwa na waandishi wa habari kama Mourinho atarejea Inter, akajibu: ‘Nammisi kama rafiki, ni mtu mzuri sana, lakini kwa sasa ana furaha anaenda Manchester.’

Bedy Moratti: ‘Mourinho va al Manchester United’ by

Jana wakati zilipotoka taarifa za Mourinho kwenda Italia kuonana na Moratti, ilibidi akanushe kwamba haendi Italia kwa sababu ya kuongelea kufundisha tena Inter Milan.


Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here