Home Ligi EPL Zlatan Ibrahimovic kujiunga na Manchester United?

Zlatan Ibrahimovic kujiunga na Manchester United?

1202
0
SHARE

zalta

Moja ya top stories mwishoni mwa msimu huu ni Ibrahimovic atasaini na club gani?. Mchezaji huyu tegemezi kwenye club ya PSG anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na bado hajasaini mkataba mpya na PSG.

Kwenye moja ya interview zake amesema kwamba kwa mtu ambae anafuatilia habari zake za mkataba mpya au club mpya basi atashangazwa na vitu vikubwa vitakavyotokea mwishoni mwa msimu huu.

Gazeti la The Mirror limeandika story ya uwezekano wa Zlatan kuungana na kocha wake wa zamani Jose Mourihno ambae walikua wote Inter Milan. The Mirror wanasema Zlatan kasema yupo tayari na fit kwa ajili ya exprience ya Premier League ambayo wachezaji wengi wanapenda kucheza.

Tetesi hizi zitapata jibu la uhakika pale Jose akichukua nafasi ya LVG kama inavyozugumzwa sasa hivi. Baada ya hatua hiyo tutasubiri habari ya pili Zlatan kutua Old Trafford.

Kwa sasa endelea kumfatilia Zlatan kwenye Ligue 1 ambayo inaonyeshwa kwenye Startimes, pia usisahau kumfatilia jobless(kwenye soka) Jose Mourihno ambae anaandikwa kwenye mitandao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here