Home Dauda TV WAANDISHI WAMVURUGA RONALDO, ASUSIA KIKAO NA KUMUACHA ZIDANE (Video)

WAANDISHI WAMVURUGA RONALDO, ASUSIA KIKAO NA KUMUACHA ZIDANE (Video)

614
0
SHARE

Ronaldo va Roma

Katika hali ya kushangaza,  mshambuliaji Cristiano Ronaldo alitoka nje ya mkutano mara baada ya waandishi wa habari kumuuliza kuhusu fomu yake ya kufunga mabao uwanja wa ugenini msimu huu, kitu kilichompelekea Ronaldo kutaka mwandishi yeyote amtaje mchezaji aliyemzidi kufunga nje ya uwanja wa nyumbani,  Ronaldo akaamua kutoka baada ya kuona hapatiwi jibu,  ingawa ilikua bado mtafsiri wa kiitaliano hajaanza kuwatafsiria waandishi.

Katika mkutano huo wa kabla ya mechi ya UEFA Champions League mbele ya Roma,  waandishi walimkalia kooni mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno,  baada ya kumtaka ajibu kuwa pengine urafiki wa karibu wa nje ya uwanja wa mahasimu wao Lionel Messi,  Neymar na Suarez unawafanya kuwa hatari zaidi ya wao wa Bale,  Ronaldo na Benzema.

Akijibu swali hilo, Cristiano alisema kuwa haoni hicho kuwa ni kitu muhimu sana kwani alitaka uthibitisho wa kuonesha urafiki wa wachezaji hao wa Barcelona nje ya uwanja.

“Ngoja niwaambie kitu kimoja, nilipokua Manchester United,  sikua naongea na Giggs,  Scholes wala Rio Ferdinand nje ya uwanja,  zaidi ya kusalimiana tu kawaida asubuhi,  lakini tulishinda ubingwa wa Ulaya.  Kwahiyo kwangu mimi hiyo sio ishu muhimu” alisisitiza Ronaldo.

Real Madrid wanancheza leo na AS Roma ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora kabla ya marudiano pale Santiano Bernabeu, huu ni mchezo wa kwanza Ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane

Cheki video hapa Ronaldo akiondoka kwenye press conference baada ya waandishi kushindwa kumjibu ni mchezaji gani aliyefunga magoli mengi kwenye viwanja vya ugenini kuliko yeye.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here