Home Ligi BUNDESLIGA PSG na Real Madrid wanamtaka Lewandowski..lakini hii ndio habari mpya.

PSG na Real Madrid wanamtaka Lewandowski..lakini hii ndio habari mpya.

599
0
SHARE

munich

Robert Lewandowski ndio jina ambalo lilikua linatajwa sana mwanzoni mwa msimu huu. Jina lake lilika kwenye vichwa vya habari kutokana na kucheka na nyavu mara nyingi.

Sasa PSG na Real Madrid wanaonyesha kiasi kikubwa wanamtaka mchezaji huyu ajiunge na vikosi vya kwenye ligi zao. Sasa hivi Robert bado yupo kwenye mkataba na Bayern Munich tangu asaini mwaka 2014 akitokea Borussia Dortmund.

Mkataba wake unamfanya akae kwenye club hiyo kwa muda wa miaka 5. Lakini habari mpya ambayo sio nzuri kwa Real Madrid na PSG ni kwamba Lewandowski ameshafungua milango ya kuzungumza kuongeza mkataba na club yake ya sasa.

Baada ya kufunga magoli 31 kwenye mechi 30, sio rahisi club ya Munich kukataa matakwa ya mchezaji huyu ambae amekua mchango mkubwa kwenye mechi zao.

Jumamosi hii Bayern Munich itacheza mechi nyingine ya kwenye ligi ya Bundeslige Vs Hoffenheim. Fuatilia mechi hii kwenye king’amuzi cha Startimes.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here