Home Kimataifa BAADA YA DILI LA KUHAMIA ARSENAL KUKWAMA, OLUNGA ASAJILIWA NA KLABU NYINGINE...

BAADA YA DILI LA KUHAMIA ARSENAL KUKWAMA, OLUNGA ASAJILIWA NA KLABU NYINGINE YA ULAYA

549
0
SHARE

Olunga

Mchezajiwa Kenya ambaye alikuwa na ndoto za kuchezea Arsenal ameamua kutimkia Sweden ambako amesaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Djurgardens.

Michael Olunga mwenye umri wa miaka 21 mwakajana mwezi wa nane alitengeneza video na kumuomba meneja wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger amsajili kutoka kwenye klabu yake ya Gor Mahia ya Kenya.

Badala yake amesaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo ya nchini Sweden.

“Anajitahidi sana, anajifunza kwa malengo mara zote anataka kujifunza ili kupiga hatua”, Mkurugenzi wa michezo Bosse Andersson alisema.

“Kwa maendeleo na mazingira yetu rafiki na yenye utulivu ya Djurgardens atajifunza na atakuwa bonge la Straika atakayeweza kucheza katika ligi kubwa Ulaya.

Hayo ndiyo matarajio ya Michael na anayosifa ya kufanya hivyo.

Olunga ambaye jina lake la utanini ‘Engineer’ kwa maana mhandisi kutokana na kuwa na Degree ya Uhandisi amesema anatambua kuwa itakuwa vigumu kuzoea mazingira haraka.

“Mwanzoni itabidi nijaribu kwenda lakini nikishazoea basi nitaendelea kufunga zaidi na zaidi. Aliiambiatovutiyaklabuhiyo”.

“Mpaka sasa nimeshacheza mechi za kirafiki tu lakini najiona ni povizuri”.

“Kila kitu kimeandaliwa vizuri uwanja wa kufanyia mazoezi upo safi, unaonekana kama upotayari kwakuchezea ligi kubwabarani Ulaya”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here