Home Dauda TV MATUKIO YALIYOJIRI NYUMA YA PAZIA PENATI YA MESSI DHIDI YA CELTA VIGO...

MATUKIO YALIYOJIRI NYUMA YA PAZIA PENATI YA MESSI DHIDI YA CELTA VIGO (Video)

766
0
SHARE

Messi-Neymar

Sasa ni dhahiri kwamba Neymar ndiye aliyepaswa kupiga pasi ya penati kutoka kwa Messi badala ya Luis Suarez katika mchezo dhidi ya Celta Vigo uliopigwa katika dimba Nou Camp.

Pengine kitu kinachorufahisha zaidi katika tukio hili liligonga sana vichwa vya habari duniani ni tahamaki ya kocha wa Barcelona Luis Enrique wakati alipokuwa akiambiwa na matabibu wa timu hiyo ambao walikuwa wakifahamu mpango mzima wa kilichokuwa kikitaka kufanywa na wachezaji hao huku Enrique akionekana kutofahamu chochote.

Kunzaia mwanzoni kabisa mwa tukio, wakati Leo Messi aliposababisha penati ile, aliwakumbatia Neymar na Suarez kwa nyakati tofauti akiwanong’oneza jambo, kwa maana wawe tayari kwa mpango wao.

Wakati huo huo bechi la ufundi la Barcelona linaingiwa na taharuki, kocha Luis Enrique anajuzwa kinachotaka kufanyika. Wakati huohuo Sergio Busquets na Jordi Alba pia wanaambiwa mpango huo.

Wakati Messi akitoa ile pasi utaona kwamba Neymar anaingia ndani ya boksi haraka lakini kwa bahati mbaya anazidiwa ujanja na Suarez (ambaye inasemekana alikuwa amesimama ndani ya D, na hivyo wataalamu wanadai kwamba goli hilo lisingeruhusiwa).

Angalia video hii hapa chini inayoonesha nyuma ya pazi ya matukio yote hayo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here