Home Kimataifa BARCA BILA YA MESSI, NEYMAR, SUAREZ, YAWEKA REKODI MPYA

BARCA BILA YA MESSI, NEYMAR, SUAREZ, YAWEKA REKODI MPYA

539
0
SHARE

Barca 3

Goli la kusawazisha la Wilfrid Kaptoum sio tu liliwanyima ushindi Valencia iliyo chini ya Garry Neville ambao ungewaongezea ari, lakini pia limeongeza idadi ya michezo ambayo Barca wamecheza bila kufungwa na kufikia michezo 29.

Barcelona ambayo ipo chini ya kocha ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo Luis Enrique hawajapoteza mchezo katika mashindano yote wanayoshiriki tangu Oktoba 3, na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Pep Guardiola msimu wa 2010/11 wakati akiifundisha klabu hiyo.

Mara ya mwisho Barcelona walifungwa na Sevilla, ikiwa imeshapita miezi minne sasa.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Kocha wa Barcelona Luis Enrique akitoa maelekezo kwa wachezaji wake

Enrique aliifikia rekodi ya Guardiola wakati huohuo akiwa anatimiza michezo 100 katma kocha wa klabu hiyo, huku akisema hicho hakikuwa kipaumbele chake.

“Msimu utakapomalizika, nitawajulisha kama tumefanya kitu chanya”, alisema Enrique pale Barca ilipokuwa imetimiza michezo 28 bila ya kufungwa wakati wallipocheza dhidi ya Levante.

“Ni vizuri zaidi kucheza michezo 100 kuliko 50, lakini mimi siangalii namba. Kikubwa kinachonivutia nini umoja uliopo ndani ya wachezaji ambao unaleta matokeo chanya”.

Barcelona watajaribu kuongeza rekodi yao ya kutofungwa michezo 30 watakapokuwa wakipepetana na Celta Vigo, klabu ya zamani aliyokuwa akiinoa Luis Enrique, ambayo iliwafunga mwanzoni mwa msimu, katika mchezo huo, washambuliaji wao hatari Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar watakuwa wamesharudi.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here