Home Kitaifa VPL INAZIBEBA, YANGA SC, SIMBA SC, AZAM FC NA KUIKANDAMIZA TOTO AFRICANS

VPL INAZIBEBA, YANGA SC, SIMBA SC, AZAM FC NA KUIKANDAMIZA TOTO AFRICANS

723
0
SHARE

 

Azam vs Simba 1

Na Baraka Mbolembole

Nani mpangaji wa mwisho wa ratiba ya mechi za ligi kuu Tanzania bara (VPL)? mwanzoni mwa msimu Simba SC ilikwenda Tanga na kucheza michezo miwili mfululizo dhidi ya timu za African Sports na JKT Mgambo, Azam FC ilikwenda Shinyanga na kucheza mechi mbili mfululizo dhidi ya Stand United kisha Mwadui FC.

Yanga pia ilikwenda Tanga na kucheza mara mbili mfululizo dhidi ya Sports na Mgambo, ikumbukwe pia walikwenda Shinyanga na kucheza gemu mbili mfululizo dhidi ya Stand United na Mwadui FC. Vipi kuhusu mechi nyingine mbili mfululizo za Simba pale Sokoine, Mbeya dhidi ya Mbeya City FC na Tanzania Prisons?

Jumamosi hii Simba watakuwa na ‘ofa’ nyingine kama hiyo katika uwanja wa Kambarage, ndiyo awali Kagera Sugar ilipendekeza kuutumia uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora kama uwanja wao wa nyumbani kufuatia uwanja wa Kaitaba, Bukoka kuwa katika matengenezo, ila majuzi Simba ilicheza na Kagera pale Kambarage.

Na sasa watacheza na Stand siku ya Jumamosi hii. Si msimu huu tu hali hiyo hujitokeza kila msimu huku wahusika wakisema ratiba hupangaliwa kutoka jiografia ya nchi. Kama ni kweli, mbona ‘fever’ hiyo hujitokeza kwa timu za Dar es Salaam tu?

Mpangilio wa mechi za mzunguko wa kwanza hutumika pia katika michezo ya mzunguko wa pili. Ili kuepusha hilo ni lazima wapangaji wa ratiba wapunguze michezo mfululizo ya timu za Simba, Yanga na Azam FC katika viwanja vya Taifa na Chamanzi, pia wazitawanye ugenini walau katika michezo yao 7 au 8 ya ugenini isiwe mfululizo katika uwanja mmoja.

Mpangilio wa sasa wa ratiba hautoi nafasi ya kupumzika kwa timu nyingine ukitoa vigogo hao watatu, na hakika jambo hilo linapunguza kwa kiasi kikubwa washindani wengi katika ligi.

Toto Africans ya Mwanza imepeleka barua ya kuomba mpangilio wa ratiba urekebishwe kwa shirikisho la soka nchini, TFF. Upande wa madai yao unaweza kuonekana hauna msingi kwa maana ni ratiba ile ile ya mzunguko wa kwanza ndiyo inayotumika katika michezo ya marejeano, lakini kwa maana ya kuleta usawa kwa kila timu naweza kuungana kwa asilimia mia moja na mwenyekiti wa klabu hiyo, Godwin Aluko ambaye ameitaja ratiba ya VPL kuwa ni mbaya.

“Mpangilio wa ratiba umebadilika, kulingana na mzunguko wa kwanza ulivyokuwa. Huu mzunguko wa pili umekuwa na ratiba mpya, tulitegemea ratiba ya mzunguko wa pili ingefuata ile ya mzunguko wa kwanza. Hii ratiba kwa kweli ni mbaya na ukiangalia inaonekana kwamba sisi hatutapumzika katika ligi yote kwa sababu tutakuwa tunakwenda kituo kimoja ugenini na kurudi nyumbbni, itakuwa kama vile sisi ni watalii katika nchi”.

“Hatuwezi kupata muda wa wachezaji wetu kufanya mazoezi, kupumzika kwani muda wote watakuwa wanasafiri. Kwa hiyo itakuwa ngumu sana kwa timu yetu kufanikiwa. Ratiba ya kwanza tulikuwa tunacheza mechi 2 nyumbani, tunasafiri tunacheza mechi 2 ugenini, tunacheza mechi 3 nyumbani, tunakwenda ugenini tunacheza mechi 3. Angalau tulikuwa na muda wa kupumzika nyumbani hata kwa wiki mbili.” ni maneno ya Aluko, mwenyekiti wa timu ya Toto Africans.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here