Home Ligi EPL TOP 5 YA MASTAR WALIOSAJILIWA KWA MBWEMBWE EPL LAKINI WAMESHINDWA KUTAMBA

TOP 5 YA MASTAR WALIOSAJILIWA KWA MBWEMBWE EPL LAKINI WAMESHINDWA KUTAMBA

700
0
SHARE

Depay 3

Memphis Depay (PSV Eindhoven kwenda MANCHESTER UNITED, paundi mil 25)

Alianza kwa kasi nzuri lakini amekuwa na wakati mgumu kadri siku zinavyosonga mbele.

Amekuwa akishutumiwa kwa kuhangaika zaidi na matumizi ya magari ya kifahari kuliko kufunga na kutoa pasi za magoli.

Mbaya zaidi ni pale alipokuwa chanzo cha timu yake kufungwa katika michezo dhidi ya Stoke City baada ya kurudisha mpira wa kichwa vibaya na kusababisha goli na Chelsea baada ya kuupokea mpira vibaya ambao ulimtoka na kupelekea madhara langoni mwake kutokana na goli lililofungwa na Diego Costa mwishoni mwa wiki hii.

Depay

Pedro (Barcelona kwenda CHELSEA, paundi mil 19)

Alianza vizuri baada ya kufunga na kutoa pasi ya goli katika mchezo dhidi ya West Brow, lakini amekuwa na wakati mgumu tangu baada ya hapo.

Ndani ya michezo 23, amefunga mara mbili tu, hivyo kuwa na wakati mgumu klabuni hapo.

Christian Benteke (Aston Villa kwenda LIVERPOOL, paundi mil 32)

Benteke amefunga magoli 7 ndani ya michezo 28. Kulingana na nafasi yake anayocheza, hii ni idadi ndogo sana ya magoli kwa mshambulizi huyo mwenye uraia wa Ubelgiji.

Nicolas Otamendi (Valencia kwenda MANCHESTER CITY, paundi mil 28.5)

Kukosekana kwa Vincent Kompany kumekuwa ni pengo kubwa kwa Manchester City, Otamendi amekuwa na wakati mgumu sana pale anapocheza bila ya uwepo wa Kompany kutokana na kupitwa kirahisi mno na washambuliaji wa timu pinzani.

Mfano mzuri ni mchezo wa wikiendi iliyopita baada ya kunyanyaswa vilivyo na washambuliaji wa Leicester City Vardy na Mahrez.

Radamel Falcao (Monaco kwenda CHELSEA, mkopo)

Baada ya msimu wake mbaya akiwa na klabu ya Manchester United, Falcao alihamia kwa mkopo kunako klabu ya Chelsea.

Tangu ajiunge klabuni hapo Falcao amefunga goli moja tu

Falcao ameachwa katika kikosi cha Chelsea kitakachocheza kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya ujio wa Alexandre Pato.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here