Home Kimataifa Ronaldo: Ni muda sahihi auzwe au aendelee kubaki Madrid?

Ronaldo: Ni muda sahihi auzwe au aendelee kubaki Madrid?

877
0
SHARE

Mnamo mwezi wa sita 2015 mtandao mmoja wa michezo wa Spain ulitoa fursa kwa wasomaji wake kupiga kuhusu uwezekano wa Real Madrid kumuuza Cristiano Ronaldo. Matokeo ya kura zilizopigwa yailkuwa – asilimia 50.04 ya wapiga kura walilipinga jambo hilo na asilimia 49.96 walikubaliana na suala hilo.

  Kilichofuata Ronaldo akamaliza msimu kwa kutwaa tuzo ya Pichichi, akiwa na magoli 48. Lakini juzi jumatatu Ronaldo alikaririwa akisema kwamba atamaliza mkataba wake wa sasa na Madrid ambao unaishia June 2018. “Baada ya hapo tutaona kitakachotokea,” aliongeza CR7. Jibu ambalo lilirudisha tena ule mjadala wa uwepo wake Santiago Bernabeu.
Baada ya mechi ya wikiendi iliyopita ambapo Luka Modric aliiongoza timu yake kushinda mechi dhidi ya Granada – mjadala umeanza kuibuka kwa kasi juu ya umuhimu wa Ronaldo katika kikosi cha Los Blancos. Hakuwa tishio lolote kwa Granada, alifichwa na walinzi wa Granada na akashindwa kufunga kwa mara nyingine tena.

  Masaa kadhaa baada ya mechi hiyo dhidi ya Granada, mwanasiasa mashuhuri Manuel Cobo, ambaye sasa ni mchambuzi wa michezo cha radio – El Larguero, alitoa maoni yake juu kiwango cha Ronaldo: “Ndani ya Real Madrid kilichokuwa muhimu kabla kilikuwa ni makombe lakini sasa inaonekana kilicho muhimu ni magoli.” Katika mjadala huo katika kipindi hicho cha michezo kukawa na mazungumzo ya mabadiliko ya nafasi anayocheza Ronaldo uwanjani, kupotea kwa uwezo wake wa kupenya ngoma za ulinzi na pia likaja suala la unri wake: miaka 31.

Mpaka sasa msimu huu, Ronaldo amefunga magoli 19 kwenye ligi, sawa na Karim Benzema na goli moja pungufu na Suarez mwenye magoli 20. Kwenye michuano ya ulaya amefunga magoli 11, sita zaidi ya Suarez na manne zaidi ya Robert Lewandoski. Lakini bado mashaka juu ya kiwango chake yanabakia.

Kuna baadhi ya wadau wanasema kwamba usajili wa Lewandoski kuja Bernabeu utakuja kuwa ndio mwisho wa Ronaldo – ambaye wanaona atauzwa tu. Wote ambao wamekuwa wakiandika juu ya kuondoka kwa mfungaji bora wa muda wote wa Madrid – wamekuwa hawasemi taarifa wanazitoa wapi, japo wamekuwa wakiziandika kwa kuonyesha wana uhakika.
Ronaldo yupo msimu wa saba na Los Blancos akiwa ameshinda kila kikombe na klabu hiyo, ameshaweka rekodi nyingi mno ambazo haziwezi kuvunjwa hivi karibuni na kubwa kuliko ya ufungaji wa bora wa muda wote – hana cha kuthibitisha mbele ya mtu yoyote juu ya uwepo Bernabeu.


Madrid na mchezaji wanahitaji kifanyike kwa faida yao wote?

I’m  

 Nini kifanyike? Kumuuza Ronaldo kutaipa faida kubwa Madrid – mauzo yake yanaweza kuingiza kiasi kisichozidi 150 million euros, au hata zaidi. Tatizo ni kwamba Real Madrid sio taasisi ambayo ina mfumo wa kushare faida, labda fedha hizo ziwekezwe katika kusajili wachezaji wapya. Kama itakuwa ndio hivyo, fedha itakopatikaba kutokana na mauzo ya Ronaldo itakuwa imetumika vyema: sehemu ya fedha hizo inaweza kutumika kumsajili Lewandoski au Hazard ambaye anaweza kugharimu kiasi cha 100 million, kinachobaki kinaweza kusaidia kusajili beki kuiongezea uinara safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Kutokuwepo kwa Ronaldo, Gareth Bale atazidi kuimarika zaidi na kuwa na uhuru zaidi katika timu. Kwa hakika hatoweza kufunga magoli mengi kama ilivyo kwa Ronaldo lakini atakuwa na Lewandoski na Benzema kwenye kumsaidia kubeba mzigo wa magoli; Benzema amejidhihirisha wazi msimu huu namna alivyo na uchu langoni, ukiwaongeza James Rodriguez, Hazard au Isco katika safu hiyo ushambuliaji – nachelea kukubali kwamba watakuwa wamefanikiwa kusonga mbele vizuri.

Kwa upande wa Ronaldo anaweza kuuzwa na kwenda PSG, katika ligi ambayo sio ngumu kufananisha na La Liga, lakini kurudi Manchester United or City ya Guardiola, lakini naamini Ligue 1 ndio mahala sahihi kwa kwenda baada ya kumalizana na Madrid.

Lakini ikitokea Ronaldo asiondoke Madrid – atakuwa anaishi kwenye kivuli chake mwenyewe – na kuwa anafananishwa na kushindanishwa na Ronaldo wa muda fulani uliopita na Ronaldo wa sasa. Ronaldo ambaye kiuhalisia tu uwezo wake aa kufunga utazidi kushuka kadri muda unavyozidi kwenda japo bado anaweza kuendelea kuwa sumu kwa mabeki japo sio kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita.

Sidhani kama Florentino Pérez yupo radhi tufike huko. Sidhani kama uwepo wa Ronaldo utasaidia kuimarika kwa Bale na Lewandoski kama atasajiliwa.
Lakini yote kwa yote ni muda sahihi umefika kwa pande zote mbili kuchukua maamuzi magumu na kuchukua hatua ambazo zitawasaidia wote Madrid na Ronaldo binafsi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here