Home Dauda TV JUMA LUIZIO: SIJUTII KUTOCHEZA SIMBA NA YANGA, MIPANGO YANGU NI KUCHEZA ULAYA

JUMA LUIZIO: SIJUTII KUTOCHEZA SIMBA NA YANGA, MIPANGO YANGU NI KUCHEZA ULAYA

788
0
SHARE
Juma Luizio-mchezaji wa timu ya Zesco United ya Zambia
Juma Luizio-mchezaji wa timu ya Zesco United ya Zambia
Juma Luizio-mchezaji wa timu ya Zesco United ya Zambia

Juma Luizio ni striker wa kitanzania anayecheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Zesco United ya nchini Zambia ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini humo.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Mtibwa Sugar ya Mkoani Morogoro anasema hajawahi kujuta wala hakuna kitu ambacho amekosa kutokana na kutocheza kwenye vilabu vikongwe nchini vya Simba na Yanga.

Luizio amesema siku zote malengo yake yalikuwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na amefanikiwa katika hilo japo bado anataka kuhakikisha anasonga mbele zaidi kwenda kwenye nchi za kisoka zaidi ya Zambia ambako yupo kwa sasa.

Sports Bar ya Clouds TV imefanya mahojiano na mchezaji huyo ambaye mara kadhaa ameitwa kwenye timu ya taifa lakini mara nyingi amekuwa akiachwa na yeye ametaja baadhi ya sababu za kutoitwa mara nyingi kwenye timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Hii hapa video jamaa akifunguka kila kitu kuanzia namna alivyoanza soka, alipo sasa na mipango yake ya baadaye.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here