Home Dauda TV ANGALIA FREE-KICK YA COUTINHO INAYOFANANISHWA NA ILE YA RONALDINHO

ANGALIA FREE-KICK YA COUTINHO INAYOFANANISHWA NA ILE YA RONALDINHO

561
0
SHARE

Philippe

Philippe Coutinho amerejea vizuri kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool usiku wa Jumanne na kuonesha ubora wake baada ya kupiga bonge la free-kick na kuifungia klabu yake bao kwenye mchezo wa FA Cup dhidi ya West Ham United.

Free-kick hiyo abayo imefananishwa na ile ya gwiji wa kibrazil Ronaldinho imemrejesha vizuri nyota huyo wa Brazil ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda muda mrefu ambaye kwa mara ya mwisho alicheza kwenye kikosi cha Liverpool mwanzoni mwa mwezi January kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Capital One Cup dhidi ya Stoke City.

Coutinho alianza kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza dhidi dhidi ya West Ham na muda mchache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili alipiga free-kick hiyo kwa kuupitisha mpira chini ya ukuta uliowekwa na wachezaji wa West Ham na kuwaacha wao wakiruka juu.

Mchezo huo wa West Ham United vs Liverpool ulimalizika kwa West Ham kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool. Mabao ya West Ham yaliwekwa kambani na Michail Antonio aliyefunga goli la kwanza huku bao la ushindi likifungwa na Angelo Ogbonna

Cheki video ya free-kick hiyo hapa chini ambayo imefananishwa na ile ambayo alishawahi kupiga Ronaldinho nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here