Home Ligi EPL ZANETTI ATOA YA MOYONI JUU YA NANI MKALI KATI YA MESSI NA...

ZANETTI ATOA YA MOYONI JUU YA NANI MKALI KATI YA MESSI NA MARADONA

645
0
SHARE

Messi-Maradona

Mjadala juu ya yupi ni bora kati ya Lionel Messi na Diego Maradona umekuwa ukiwasumbua watu vichwa kwa miaka kadhaa sasa, lakini mchezaji wa zamani wa Argentina Javier Zanetti amesisitiza kuwa hakuna haja ya kuwafananisha wawili hao.

Maradona amebaki nembo na nguzo ya dunia, akiwasaidia Argentina kutwaa ndoo ya dunia mwaka 1986 na kuifikisha nusu fainali mwaka 1990, vile vile kushinda mataji mawili ya Serie A akikipa kunako klabu ya Napoli.

Wakati Messi akiwa bado hajatwaa kombe la dunia, alifanikiwa kuwafikisha ‘Albiceleste’ fainali ya kombe la dunia mwaka 2014 huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia ‘Ballons d’Or’ mara tano vile vile Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne na mataji saba ya La Liga akiwa na klabu ya Barcelona.

Zanetti, ambaye kwa sasa ni makamu wa rais wa Inter, alicheza na Messi katika timu ya taifa na akacheza tena dhidi yake akiwa Inter wakati walipokutana na Barcelona katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Amesema mshambulizi huyo hahitaji kushinda kombe la dunia kuthibitisha ubora wake wa kipaji chake.

“Mimi sielewi kwa kweli ufanano kati ya watu hawa wawili,” Zanetti alisema.

“Nadhani Diego alikuwa ni wa namna ya kipekee na vivyo hivyo kwa upande wa Messi. Ni kipi unachoweza kusema juu ya Messi? Kijana ambaye ameshinda tuzo tano za Ballon d’Or, Ligi ya Mabingwa mara nne na kufunga magoli 97 kwa mwaka.

“Hakuna haja ya yeye kushinda kombe la dunia ili authibitishie ulimwengu juu ya hilo.

“Messi balozi wa Argentina, na ninajivunia kuwa naye taifa moja la Argentina.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here