Home Kimataifa TAARIFA MPYA KUHUSU MESSI NA TATIZO LA FIGO

TAARIFA MPYA KUHUSU MESSI NA TATIZO LA FIGO

743
0
SHARE

Leo Messi 2

Hapo awali iliarifiwa kuwa Lionel Messi angefanyiwa upasuaji ili kuondoa tatizo la figo linalomkabili nyota huyo.

Mshambulizi huyo nyota wa Barcelona alikosa baadhi ya michezo ya Ligi ya Vilabu Bingwa Duniani kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya figo, hivyo klabu yake kuthibitisha kwamba angefanyiwa vipimo jana Jumatatu.

Barca wanatarajia kumwona Messi akirudi mazoezini Jumatano wiki hii, hata hivyo, watu wa karibu na nyota huyo vimethibitisha kuwa suala hilo bado halijafanyiwa maamuzi.

“Taarifa hizi juu ya upasuaji hazina ukweli wowote”, chanzo kilisema. “Kikubwa ambacho atafanyiwa ni kuangaliwa mwenendo wa afya yake na kufanyiwa matibabu ya figo ambayo yanamsumbua.”

Taarifa hizi ni pigo kubwa kwa mashabiki wa Arsenal baada ya hapo awali kuripotiwa kwamba endapo Messia angefanyiwa upasuaji huo, basi angekaa nje kwa kipindi kirefu na hivyo kuukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal. lakini kwa mujibu wa taarifa hizi mpya, Messi ataendelea kutoa huduma kama kawaida kunako klabu yake pendwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here