Home Kimataifa SAMATTA: VIONGOZI WAMENIAMBIA NIMECHEZA VIZURI KWA MUDA MFUPI

SAMATTA: VIONGOZI WAMENIAMBIA NIMECHEZA VIZURI KWA MUDA MFUPI

795
0
SHARE
Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk looks behind him during the Jupiler Pro League match between Royal Mouscron Peruwelz and KRC Genk in the Le Canonnier Stadium in Mouscron, Belgium. *** MOUSCRON, BELGIUM - 06/02/2016 Photo by Nico Vereecken / Photonews ***
Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk looks behind him during the Jupiler Pro League match between Royal Mouscron Peruwelz and KRC Genk in the Le Canonnier Stadium in Mouscron, Belgium. *** MOUSCRON, BELGIUM - 06/02/2016 Photo by Nico Vereecken / Photonews ***
Photo by Nico Vereecken / Photonews

Mbwana Samatta kwa sasa maisha yake ya soka yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na alivyokuwa TP Mazembe pale nchini Congo DR. Kwa sasa ameanza maisha mapya nchini Ubeliji tangu aliposajiliwa na klabu ya Genk.

Samatta ameeleza changamoto ambazo amekuwa akikabiliana nazo tangu atue Genk, Jumatatu February 8 alifanya mahojiano ya moja kwa moja na Sports Bar ya Clouds TV kupitia Skype na kufunguka mambo kibao ambayo kama mdau wa michezo ni vyema ukapata kujua.

Sports Bar: Mechi ambayo ulicheza kwa mara mara ya kwanza wakati timu yako inapata ushindi wa goli 1-0 ugenini, ulitarajia kama ungepangwa kwenye mechi hiyo?

Samatta: Sikujua ilikuwaje na kocha alifikiria nini, kwasababu kabla ya hapo tulishaongea kwamba hata nitumia kwenye mechi hiyo na atanitumia kwenye mechi nyingine. Lakini siku ya mwisho ambayo tulimaliza mazoezi (Ijumaa) kabla ya mchezo wa Jumamosi aliniambia ntakuchagua kesho twende pamoja katika hiyo mechi.

Hauwezi kukataa kwasababu alikwambia sitokuchagua na baadae amebadilisha, yeye ndiyo mwalimu muhimu ni kwamba niko tayari kwahiyo chochote kitakachotokea kwa muda wowote nafikiri nitakuwa tayari.

Sports Bar: Kocha wako Peter Maes alikwambia nini wakati unaingia kipindi cha pili dakika ya 73 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis?

Samatta: Timu ilikuwa iko mbele kwa ushindi wa goli 1-0 na alichoniambia ni kwamba tunahitaji kulinda ushindi, chochote kitakachotokea vyovyote itakavyokuwa lakini nihakikishe timu inacheza pamoja ili tusipoteze ushindi.

Sports Bar: Baada ya mechi kumalizika ulipata comments gani kutoka kwa mwalimu na hata viongozi wa timu?

Samatta: Viongozi walinipa feedback ya mchezo waliniambia nimecheza vizuri kwa muda mfupi lakini nilionesha kwamba nilikuwa na nia ya kujituma kwasababu muda mwingi nilikuwa nakimbia najaribu kuisaidia timu pia rais wa timu nilikutana naye na alinipongeza pia.

Sports Bar: Upo ugenini, ukitoka mazoezini huwa unafanya kitu gani ambacho kinakufanya uwe busy muda mwingi?

Samatta: Nikitoka mazoezini mara nyingi huwa nikirudi nyumbani naabgalia TV, nacheza PlayStation, nasikiliza music na vitu vingine vingi ambavyo vinanifanya muda mwingi niwe busy. Huku muda wa jua ni mchache saa 12:00 jua linakuwa limeshazama na linachomoza kuanzia saa 2:30 au saa 3:00 kwahiyo muda wa kulala kwangu unakuwa ni mchache kwasababu nakua nafanya vitu vingi.

Sports Bar: Kitu gani kwa sasa ambacho ni changamoto kwako tangu umefika ubelgiji?

Samatta: Kwakweli kwasasa nafikiri ni ugeni, ugeni ni changamoto kubwa kwasababu mazingira mengi sijayazoea nahitaji kuzoea ili vitu vingine viwe rahisi. Kingine ni hali ya hewa kidogo bado inanipa shida lakini nikishazoea vitu hivyo kila kitu kitakuwa sawa.

Sports Bar:Kwasasa unaishi wapi, kambini, hotelini au umepangishiwa nyumba?

Samatta: Kwasasa mimi naishi kwenye apartment ambayo hata sijui ni mtaa gani kwasababu bado ni mgeni na niko pekeyangu. Nipo hapa sijui ninaishi eneo gani. Kilasiku wanakuja kunichukua hapa kunipeleka mazoezini na kunirudisha.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here