Home Entertainment Ronaldo na Messi kwenye vita ya ununuzi wa Ferrari Ghali Zaidi! Mmoja...

Ronaldo na Messi kwenye vita ya ununuzi wa Ferrari Ghali Zaidi! Mmoja atajwa kushinda 

1461
0
SHARE

Wanasoka bora zaidi katika kizazi hiki cha soka cha sasa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wametajwa kuingia kwenye ushindani mwingine usiokuwa rasmi wa kuinunua gari aina ya Ferrari ambayo inatajwa kuwa ya ghali zaidi katika historia ya utengenezaji aa magari hayo.

  Imeelezwa kwamba gari ya Ferrari ya ghali zaidi iliyokuwa ikimilikiwa na taasisi ya Proto, ambaye mmiliki wake, Alessandro Proto – aliiweka mnadani gari hiyo aina ya Ferrari 335 S Spider Scagliettu jijini Paris na hatimaye ikauzwa kwa kiasi cha 32 million euros.
Mpaka sasa mnunuzi wa gari hilo jina lake halijawekwa wazi, lakini kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na kampuni ya Proto inaonekana gari hilo limenunuliwa na Messi.

  Proto Organisation pia wameonyesha kwamba Cristiano Ronaldo alikuwa nae analitaka gari hilo ambalo liliwahi kuendeshwa na Sterling Moss katika mashindano ya magari ya Cuban Grand Prix mnamo mwaka 1958, lakini Messi akashinda vita ya ununuzi wa ndiga hiyo.

Mnada wa gari hilo ulianzia kwa bei ya 20 million euros na ukaishia kwenye bei ya 32 million euros, bei ambayo ni rekodi ya juu ya mauzo ya gari za aina hiyo. Hata hivyo vyanzo vilivyo karibu na mchezaji vimekanusha juu ya biashara hiyo.

Alessandro Proto, ambaye aliuza gari hiloni milionea wa kiitaliano ambaye alitaka sana jina lake lipate vichwa vya habari hivi karibuni – pia ndio mtu ambaye amemuuzia Florentino Perez apartment ya kifahari jijini New York ambayo ina thamani ya 60 million euros. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here