Home Ligi EPL MZIMU WA MOURINHO UNAENDELEA KUMTESA VAN GAAL

MZIMU WA MOURINHO UNAENDELEA KUMTESA VAN GAAL

571
0
SHARE

Van Gaal +Mourinho

Kocha wa Manchester United mholanzi Louis Van Gaal jana ameendeleza vita yake na waandishi wa habari nchini England baada ya kuulizwa swali kuhusu ujio wa Jose Mourinho Old Trafford

Van Gaal alikasirishwa na swali aliloulizwa na mwandishi mmoja wa habari kuwa kiwango kizuri kinachooneshwa na timu yake kwa sasa ni kwa sababu kuwa klabu inajiandaa kumtangza mrithi wake?

Akiwa katika hali ya hasira baada ya timu yake kulazimishwa sare ya goli 1-1 dhidi ya Chelsea, asante kwa goli la Diego Costa katika dakika za lala salama Van Gaal alikuwa na haya ya akujibu

“Mmeshaongea na Ed Woodward? alisema. Kwanini wakatae (tetesi kuhusu Mourinho?) siingilii pia. Sasa kwanini klabu ikatae kuhusu hilo. Wakati mnatengeneza habari?”

“Sawa. kwahiyo hamkuongea na Ed Woodward, na hamkuongea na familia ya Glazers pia kwahiyo mmetengeneza habari. Halafu mnataka mimi nijibu hili swali. Sijibu hili swali. Na ntarudia kila wiki “.

“Sasa labda niseme kuwa wote mnafukuzwa kesho. Mnaitwa kina nani? halafu natangaza majina yenu. Waangalieni wake zenu au watoto wenu au binamu zenu na watu wengine kama hao”.

Kwa sasa Van Gaal yupo katika wakati mgumu kutokana na timu yake ya Manchester United kutocheza na kupata matokeo mazuri kama inavyotarajiwa na mashabiki wake huku idadi kubwa ya mashabiki pamoja na wachezaji wa zamani wa Klabu hiyo wakitaka Van Gaal atimuliwe katika kiti hicho cha Old Trafford

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here