Home Ligi EPL MATA AWAKUMBUSHA MBALI MASHABIKI WA CHELSEA

MATA AWAKUMBUSHA MBALI MASHABIKI WA CHELSEA

514
0
SHARE

Mata Juan 1

Baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mechi (Man of the Match) kwenye sare ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Manchester United, Mata alifanya tukio ambalo liliwakumbasha mbali mashabiki wa Chelsea mara baada ya filimbi ya mwisho.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alisalia uwanjani na kupeana mkono na wachezaji wote wa Chelsea baada ya mchezo kumalizika.

Mata Juan 2

Akiwa Chelsea mashabiki walimchagua  mara mbili kuwa mchezaji bora wa mwaka. Mata bado anakumbukwa na kupendwa na mashabiki wa timu yake ya zamani hasa kutokana na nidhamu ambayo amekuwa akiionesha kwa wachezaji wenzake wa zamani kila anapokutana nao.

Mata aliondoka Stamford Bridge mwaka 2014 kutokana na ujio wa kocha wa zamani wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye hakuhitaji huduma ya mhispania huyo.

Mata Juan

Lakini Mourinho pia yupo nje ya Chelsea, Mata ameonekana alikuwa mwenye furaha kukutana tena na wachezaji wenzake wa zamani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here