Home Ligi EPL MOURINHO KURUDI KAZINI HIVI KARIBUNI?, MWENYEWE AMEWEKA WAZI KILA KITU

MOURINHO KURUDI KAZINI HIVI KARIBUNI?, MWENYEWE AMEWEKA WAZI KILA KITU

597
0
SHARE

Mo 8

Jose Mourinho amesema yuko mbioni kurejea kundini huku akisisitiza kuwa atabaki nchini Uingereza.

Mara kadhaa vyombo mbalimbali vya habari nchini Uingereza, vimekuwa vikimhusisha Mourinho kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Manchester United.

Katika moja ya mahojiano aliyofanyiwa hivi karibuni Mourinho amesema: “Ili kuwa na furaha iliyokamilika, nahitaji kuwa na kila kitu, hivyo nataka kurejea kwenye soka. Nadhani ndio kitu napenda zaidi. Nimefanya kazi kama Meneja tangu mwaka 2000. Kimsingi nitarejea kundi hivi karibuni,” alisema.

 Jana Mourinho alionekana akiwa jukwaani nchini Ujeruamani akiangalia mchezo kati ya Hertha Berlin na Dortmund
Jana Mourinho alionekana akiwa jukwaani nchini Ujeruamani akiangalia mchezo kati ya Hertha Berlin na Dortmund

Aliongeza kuwa: “Kwa wakati huu sina kazi yoyote, na sijui nitaelekea wapi, kwa sababu kwenye mchezo wa mpira wa miguu lolote linaweza kutokea. Lakini, kwa kukuhakikishia, kama familia, maisha yetu yatabaki kuwa nchini England.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here