Home Dauda TV VIDEO: MASHABIKI WA LIVERPOOL WAGOMA NA KUTOKA NJE YA UWANJA, TIMU YAO...

VIDEO: MASHABIKI WA LIVERPOOL WAGOMA NA KUTOKA NJE YA UWANJA, TIMU YAO YABANWA UNFIELD

639
0
SHARE

Liverpool-mgomo

Juma lililopita klabu ya Liverpool ilitangaza bei mpya ya ticket kwa ajili ya msimu ujao na mashabiki wa timu hiyo wameamua kupinga hatua hiyo iliyochukuliwa na klabu yao.

Klabu hiyo imepanga mashabiki wake walipe kiasi cha £77 ikiwa ndiyo kiwango kikubwa cha bei ya ticket ya jukwaa kuu.

Liverpool-mgomo 2

Mashabiki wa klabu hiyo katika kuonesha kwamba hawakubaliani na mpango huo wa klabu yao, waliingia na vipeperushi pamoja na bendera nyeusi kwenye uwanja wao wa Unfield wakati wa mchezo wa timu yao dhidi ya Sunderland uliomalizika kwa timu hizo kufungana kwa bao 2-2.

Moreover, when the 77th minute of the match came around, the fans left Anfield in huge numbers.

Ilipofika dakika ya 77, mashabiki wakiwa kwenye makundi makubwa walianza kutoka nje ya uwanja wa Unfield.

Matokeo ya mechi zote za EPL zilizochezwa leo February 6, 2016

EPL Feb 6

Video namna ambavyo mashabiki wa Liverpool walivyotoka nje ya uwanja kupinga bei mpya ya viingilio kwa ajili ya msimu ujao

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here