Home Ligi EPL Kwanini Mourinho Ndio Mtu Sahihi kwa Man Utd – Baada ya City...

Kwanini Mourinho Ndio Mtu Sahihi kwa Man Utd – Baada ya City Kumpata Guardiola 

708
0
SHARE

Wakati tangazo la kumuajiri Pep Guardiola lilipotolewa na Manchester City  hakukuwa na mshangao wowote. 
Lakini kwa mashabiki wa Manchester United ilikuja kwa kuwaongezea mawazo juu ya hatma ya klabu yao siku za mbeleni. 
Hawajawahi kuonekana kama wana uwezo wa kushindania taji tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson.

  Na sasa watakuwa wakishuhudia kocha bora duniani akichukua majukumu ya kuifundisha Manchester City. 

Louis van Gaal kwa kujiamini kabisa amekuwa akisema United haitokumbwa na ukame wa mataji kama ilivyo kwa Liverpool. 

Lakini kikosi cha Van Gaal hakionyeshi matumaini yoyote ya kupanda kwenye jukwaa la washindi aa kombe lolote katika siku za hivi karibuni.

Kwa United msimu huu kupata nafasi ya kumaliza nafasi ya 4 itakuwa ni mafanikio makubwa. 

Baada ya hapo msimu ujao watakutana na upinzani mpya wa majirani zao City itakayokuwa ikiongozwa na kocha aliyeshinda kila kombe katika ngazi ya klabu – Pep Guardiola. 

Kuna mtu mmoja tu ambaye atakayeweza kupambana vyema na kocha huyo wa kihispaniola na si mwingine bali ni Jose Mourinho. 

  Kwanini Mourinho?

Watu wengi wanadhani kwamba alimshindwa Guardiola wakati walipokuwa Spain. Lakini ikumbukwe Mourinho alishinda kila taji la nyumbani katika miaka yake miwili ya mwanzo ya Real Madrid – likiwemo taji la mwaka 2012 – ambapo aliiongoza Los Blancos kutwaa ubingwa wakiwa na tofauti ya pointi 9 na Barca ya Guardiola.

Katika kufanikisha hilo aliweka rekodi kadhaa kwa kutwaa ubingwa kwa pointi nyingi(100 points) zaidi kuliko timu yoyote katika ligi kubwa barani ulaya, akishinda mechi nyingi zaidi kwenye La Liga – mechi 36, na ushindi wa mechi nyingi ugenini – akishinda mechi 16.

Pia timu yake ikimaliza kwa kufunga magoli mengi zaidi ulaya, magoli 121 – tofauti ya magoli ilikuwa 89. 

Mambo hayakuisha vizuri Santiago Bernabeu, lakini sio mara zote amekuwa akimaliza vibaya, angalia ilivyokuwa Porto, au Inter Milan ambapo alishinda ubingwa mwingine wa ulaya.

Kwa hakika atakuwa amejifunza kwa kile kilichotokea katika awamu yake ya pili ndani ya Chelsea. Mourinho anafahamu nini United inataka na hivyo kuna baadhi ya tabia zake hatokuwa na namna zaidi ya kuziacha.

  United wamepoteza nafasi ya kumpata Guardiola, sasa hawawezi kuacha fursa ya kumsajili kocha anayeweza kupambana na mhispaniola huyo na kumzidi maarifa – JOSE MOURINHO. 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here