Home Kimataifa KLABU YA CHINA YANASA SAINI YA MBRAZIL ANAYEWANIWA NA LIVERPOOL

KLABU YA CHINA YANASA SAINI YA MBRAZIL ANAYEWANIWA NA LIVERPOOL

507
0
SHARE

Alex Teixeira 1

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Shakhtar Donesk ya Ukraine Mbrazil Alex Teixeira ambaye alikuwa anawindwa na Liverpool katika dirisha dogo la mwezi Januari sasa atajiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya huko nchini China.

Taarifa zilizothibitishwa na mtandao wa klabu ya Shakhtar Donesk zinasema kuwa Teixeira atajiunga na Jiangsu Suning kwa ada ya Euro milioni 38

Klopp na Liverpool yake kwa sasa hawana nafasi tena ya kumsajili kiungo huyo mshambuliaji ambaye pia anaweza kucheza nafasi ya winga ya kushoto na kulia

Teixeira anaungana na Mbrazili mwenzie Ramires ambaye ametimka Chelsea hivi karibuni na atakuwa chini ya meneja ambaye ni beki wa zamani wa chelsea Dan Petrescu.

Teixeira ambaye alikaririwa na mtandao wa habari za michezo wa England Sky Sports katika majira ya dirisha dogo akiwa na klabu yake ya Shakhtar Donesk katika mapumziko kule nchini Marekani alionesha nia ya kujiunga na majogoo wa jiji Liverpool lakini dili lilishindwa kukamilika kutokana na Liverpool kushindwa kukamilisha ada iliyokuwa inahitajika na Shakhtar Donesk.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here